Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
Tangu vita dhidi ya Ufisadi ianze hapa Afrika mashariki, sijasikia mwanamke yeyote aliyetajwa kuwa FISADI.
Hii inanifanya nifikiri kuwa huenda wanawake ni watu waaminifu sana wakipewa uongozi wa juu katika nchi.
Labda wanawake ni waaminifu sana kutunza dhamana ya madaraka wanayokabidhiwa.
Au mnasemaje wanajamii?
wanawake wanaweza kuwa mafisadi kwa kuuma na kupuliza kama panya...
mfano mama yetu wa bunge a afrika aliyelazimishwa kujiuzulu...
ufisadi wa akina baba ni wa kubugia kila kitu kwa haraka haraka mpaka mwenye mali kustuka...mfano mzee wa viji-cent
Lakini usisahu, takribabani kwa kila mwanaume, nyuma yake kuna mwanamke!
Lakini usisahu, takribabani kwa kila mwanaume, nyuma yake kuna mwanamke!
NONO,
MSEMO huo hauhalalishi kuwa wanawake wanahusika moja kwa moja katika ufisadi.
Mbona hatusikii tuhuma za moja kwa moja?
Bado kuna jambo la kufikiria hapa.
Mkuu umeshaambiwa kuwa Mama Mongela ametajwa na amelitia hasara Taifa, unataka wengine zaidi? Unamkumbuka yule dada liyefikishwa mahakamani kwa wizi wa fedha za EPA, au yule aliyehongwa kwenye kashafa ya IPTL. Wapo, usidhani kama wao nido wasafi kuliko wanaumwe. Kuna wengi tu, hata wezi kama S.M Simbaulanga. Hakuna cha kufikiri wapo wengi tu, nenda mawizarani ukasikie mambo utajua.
kwa hiyo mnapendekeza mfumo JIKE uchukue nafasi katika madaraka nchini Tanzania?
au kuna maana nyingine zaidi ya hiyo?