hakuna mwanangu atakaekanyanga shule za serikali

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
hakuna cha shule ya wenye vipaji maalumu,sipo tayari kuangamiza ubongo wa watoto kisa shule uchwara za serikali,nataka watoto wangu wapate ufahamu sahihi hata kama wana div3
 
unasema hivyo kwakuwa una shilingi, ukiyumba kiuchumi utabadili usemi
 
Wewe unadhani siye wengine tunaosemesha shule za kata tulipenda?
 
Kama kilaza?
vilaza ndio wanaendaga shule za private mana hawachaguliwi,hata mimi nilikuwa kilaza mana sikuchaguliwa form one,ila walinitoa ukilaza wote nikawa on fire
 
hakuna cha shule ya wenye vipaji maalumu,sipo tayari kuangamiza ubongo wa watoto kisa shule uchwara za serikali,nataka watoto wangu wapate ufahamu sahihi hata kama wana div3

Div iV ya 43 ina-apply hata uko utakapompeleka unless ni international school or Nje ya Tanzania.
 
unasema hivyo kwakuwa una shilingi, ukiyumba kiuchumi utabadili usemi
kuna shule zinatoa best education with very affordable fee,sema watu hamtaki kufatilia,mfano shule niliyosoma haina ada kubwa pamoja na kung'aa muda mrefu,mpaka sasa ada ya boarding haifiki 700,000 kwa mwaka form one to form six.
 
Shule gani hiyo?
 
Div iV ya 43 ina-apply hata uko utakapompeleka unless ni international school or Nje ya Tanzania.
huko nitakapompeleka div 4 ni msamiati,wanafunzi hawaelewi,na kwa madaraja haya mapya div 3 ndo vilaza pale,wengi One na two,tofauti ya mwanafunzi wa private ni kubwa ukimlinganisha na wa serikali hata kama wanalingana matokeo kuangalia uelewa wao
 
Wewe unadhani siye wengine tunaosemesha shule za kata tulipenda?
inawezekana hukupenda,lakini wazazi wengi wanaleta mzaha kwenye elimu,wanaendekeza starehe kuliko elimu ya watoto,wengine hawaelewi elimu sahihi kwa watoto wao pamoja na kuwa na uwezo
 
Muulize Ada ya mwaka gani hiyo?usikute unaongea na mtoto hapa anakenga maghorofa hewani
mpaka sasa kuna wadogo zangu wawili pale,form six na form three,ada ndo hiyo current,mimi nilisoma hapo na kumaliza in mid 2000s na ada ya boarding ilikuwa 300000 mpaka 2006
 
Hakuna mzazi anapenda shule za kata ni umasikin tu. Kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba zake
 
hakuna cha shule ya wenye vipaji maalumu,sipo tayari kuangamiza ubongo wa watoto kisa shule uchwara za serikali,nataka watoto wangu wapate ufahamu sahihi hata kama wana div3

Labda uwapeleke nje ya nchi..!! Kama watasoma hapahapa watatungiwa mitihani na serikali ya division 5 hii hii...!!!!
 
huko nitakapompeleka div 4 ni msamiati,wanafunzi hawaelewi,na kwa madaraja haya mapya div 3 ndo vilaza pale,wengi One na two,tofauti ya mwanafunzi wa private ni kubwa ukimlinganisha na wa serikali hata kama wanalingana matokeo kuangalia uelewa wao

Tuna ma-private schools meeeeengi...!!! Lakini sijapata kusikia mtanzania/mprivate amebuni chochote hata injini ya kidampa...!!! So watz wote nawaona kuwa ni vilaza tu...!!!
 
Muulize Ada ya mwaka gani hiyo?usikute unaongea na mtoto hapa anakenga maghorofa hewani

Yeah nahisi kitu kama hicho....... Anaweza akawa mtoto. Anadhani shule za vipaji maalum au za kawaida zilikuwa na walimu au tution ndo zilikua zinatoa watu. Anyway inaonekana ameshindwa kutaja hiyo shule coz watu watakuja na analysis ya miaka 10 iliyopita.
 
Back
Top Bottom