Hakuna Taifa lenye Amani duniani chini ya ''mabeberu''.Amani ya nchi huamuliwa na ''Mabeberu''

Hakuna Taifa lenye Amani duniani chini ya ''mabeberu''.Amani ya nchi huamuliwa na ''Mabeberu''

undefine

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
442
Reaction score
1,011
Dunia ya sasa inaendeshwa na Petrol ''Dollar'' Petrol ndiyo inayo determine thamani ya Dollar.
unaweza kujiuliza ni kwanini USA ni super power mpaka sasa hivi na kwanini isiwe Urusi?
wapo wanaowasifia Urusi kwa uwezo wa kijeshi,ujasusi lakini bado Urusi atabakia kuwa mdogo kwa USA.

USA anacontrol 'petrol' utake usitake uchumi wa dunia ni USA anaye uendesha na kuusimamia.
Petrol ni silaha kubwa sana ndio maana unaona Saudia Arabia na USA ni washirika na marafiki wakubwa sana.Saudia amemuachia USA aiendeshe Petrol na USA akiamua kuiyumbisha dunia hashindwi.Petrol ndiyo inayothaminisha 'Dollar'.Ukiona Dollar imepanda fahamu ya kwamba mafuta ndiyo imesababisha Dollar ipande na ukiona Dollar imeshuka fahamu ya kwamba Mafuta ndiyo imesababisha Dollar ishuke.

USA ''Bepari'' sera yake kubwa ni kusambaza demokrasia kwa nchi zote na nchi zinazokiuka demokrasia huwekewa vikwazo mbali mbali.Nchi nyingi ambazo zilikuwa na utofauti na 'Mabepari' USA mwisho wao tumeouona

.Iraq- Saddam alikuwa jeuri kwa mabepari mwisho wa siku alidhalilishwa,Ghaddafi alikuwa jeuri kwa mabepari hakutaka kufuatisha mabepari walichotaka.Hakutaka kuendana na bei ya mafuta ya mabepari alikuwa anajipangia mwenyewe mwisho wa siku Mabepari walimdhalilisha.,Iraq war tumeona matank ya mafuta mengi yakichukuliwa na mabepari.,libya saizi matank ya mafuta kila siku yanapelekwa nje

CIA wana njia nyingi sana ya kukuadhibu

1.wananunua media na kusambaza propaganda
2.wanawanunua maofisa wakubwa wa jeshi mfano mapinduzi ya mwaka huu Uturuki
3.wanawanunua Usalama wako wa taifa,wanasiasa nk
4.wanatengeneza makundi ya waasi na kuwasambazia silaha

Venezuela-ni nchi inayomiliki hazina ya mafuta lakini viongozi wao Hugo Chavez na Nicolas Maduro wamekuwa wapinzani wakubwa wa ''mabepari'' USA leo hii mafuta haiwasaidii chochote.Leo hii venezuela wanapanga foleni kununua mswaki,mshahara wa mwezi ndio unatumika kununua chakula.Wafanyakazi wanafanya kazi bure sababu mshahara wanaopata hutumika kwenye chakula tu.na hawa viongozi walipata majaribio mengi ya kuuwawa.

*Chavez alikataa makampuni ya west yachimbe mafuta katika ardhi ya Venezuela akikataa katakata kuuza ardhi yake kwa mabepari na ukizingatia yeye ni anti capitalism na anti west kilichofuata USA wakawa wanawa-Finance oppositions ili wachukue nchi na wakishachukua nchi waingize Sera zao na kuanza kuchota mafuta njia hiyo ilifeli sababu Chavez ni kipenzi cha wanavezuela kila chaguzi alikuwa anashinda kwa kishindo baadae wakaiwekea vikwazo Venezuela ili watu wamtose Chavez lakini ilishindikana sababu Chavez alikuwa kama nabii nchini Venezuela baada ya kuona options zote zimeshindikana wakampa cancer na akafa Chavez ,Leo hii Maduro kashindwa kui-controll Venezuela kama mtangulizi wake nchi inamfia .


CONGO -Kuna hadhina kubwa sana ya madini lakini kila uchwao kuna makundi mengi ya waasi ,baadhi ya NGO's walioenda kule wanasema USA ndio wafadhili wakubwa wa waasi,magari ya UN yamekuwa yakionekana yakibeba silaha na inataarifiwa ndio wasambazaji wa hizo silaha huku madini yakichotwa na Mabepari.

SYRIA-Bashar Al Assad ni mshirika mkubwa wa urusi na tunafahamu nchi ya syria ina hadhina kubwa ya mafuta na Gas .USA aliingia kati kwa kudai Syria hakuna democrasia sababu Assad amekaa madarakani kwa kipindi kirefu laini wanasahau ya kwanba Saudia Arabia inaongozwa na familia ya kifalme.Kwanini Saudia haguswi na syria aguswe jibu ni sababu Assad yupo upande wa urusi.USA amefadhili makundi mengi ya waasi kwa kuwapa silaha,pesa nk sababu kubwa aweke pandikizi kwa bendera ya Democrasia ili mafuta,Gas imilikiwe na Mabepari/

UKRAINE- Ukraine ni nchi inayoongoza kuwa na Gas na tumeona namna mataifa makubwa yakigombana sababu ya Ukraine ''GAS'' mpaka vita viliibuka.



Ukiona nchi ina mali asili aidha mafuta,Madini na haina machafuko basi fahamu taifa hilo linatii matakwa ya mabepari na mataifa mengi yaliyokumbwa na machafuko sababu kubwa ni viongozi wamekataa kufuata matakwa ya mabepari.Ukijifanya mbishi kuzuia mafuta,madini zako zisitoke utaundiwa zengwe tu .Watafanya juu chini kiongozi aliyopo madarakani atolewe kwa njia yeyote ile aidha kununua wasaliti ,wataendesha propaganda nyingi kwenye media,hata kuunda makundi ya waasi wataunda na wakishindwa kama ilivyokuwa kwa Fidel Castro,Chavez,basi utawekewa vikwazo vya kila aina.




Tuvute picha endapo Tanzania,Kenya,Angola tungeamua tusichimbe madini tuyaache ardhini au iundwe sera ya kuhodhi rasili mali hizi.Nini kitakachotutokea Mabepari wataweza kutuacha hivi hivi.

Ukiona taifa Lina amani fahamu Mabepari wameamua iwe hivyo


Freedom in capitalist society always remains about the same as it was in ancient Greek Republics.Freedom for slave owners-Vladimir Lennin

so long as the state exists there is no freedom.When there is freedom,there will be no state.-Vladimir Lennin

HAKIKA VLADIMIR LENINN ALIKUWA GENIUS
 
Mimi nadhani umaskini ndio mama wa mabalaa yote duniani.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe hasa barani Africa chanzo ni umasikini.
 
Sasa kama ukraine ana gas ilikuwaje Russia akawa anatishia kumsambazia gas kipindi cha majira ya baridi kisa ikiwa ni deni ambalo alikuwa anadaiwa halafu suala la syria kinachotafutwa pale ni bomba la gesi kutoka Qatar kwenda ulaya kitu ambacho hataki kukiona na kikwazo ni Bashar aligoma lisipite kwake
 
Sio USA tu, unamsahau na China.
Influence ya China ni kubwa sana, US yenyewe inaitegemea China sana. Tupo kwenye situation ambayo China ikiyumba dunia nzima inayumba sawa na US tu.
 
Leo nimeona Taiwan kapitisha sheria ya kuoa mashoga, na ndio nchi ya kwanza kwa bara la Asia,hatari sana hawa wajamaa wa demokrasia
Nalog off
 
Hakuna haja ya kuogopa, kuna msemo wasema waoga hufa mara nyingi kabla ya kile kifo halisi.
Kikubwa ni kuwa wamoja na kushikamana[uzalendo] tazama Korea Kaskazini, Cuba raia wanajua viongozi wanaowaongoza ni wazalendo na wote kwa pamoja wanalinda mataifa yao dhidi ya mabaradhuli wa dunia hii na wanakataa hii ya kuamuliwa mambo yao na mabeberu.
Unamwambia Magufuli watch out sasa je rais Durtete wa uphilipino utamwambiaje?
Duniani ni mapambano mkuu.
 
We utakuwa huelewei bora ukae kimya

Sio USA tu, unamsahau na China.
Influence ya China ni kubwa sana, US yenyewe inaitegemea China sana. Tupo kwenye situation ambayo China ikiyumba dunia nzima inayumba sawa na US tu.
 
Sio USA tu, unamsahau na China.
Influence ya China ni kubwa sana, US yenyewe inaitegemea China sana. Tupo kwenye situation ambayo China ikiyumba dunia nzima inayumba sawa na US tu.
Fafanua kidogo mkuu
 
Back
Top Bottom