SoC04 Hakuna Tanzania Bora bila ya kizazi bora

SoC04 Hakuna Tanzania Bora bila ya kizazi bora

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 24, 2024
Posts
9
Reaction score
7
Kwa kiasi kikubwa haiwezi kupingika ya kuwa ili tuwe na Tanzania bora tunayohitaji lazima tuweke nguvu kubwa katika swala zima la malezi ya watoto na vijana kwani wao kwa kiasi kikubwa ndio wanaongoza katika suala zima la ujengaji wa nchi.

Kama Tanzania ili tuendelee kuwa na nchi nzuri na salama lazima kuwe na kizazi bora ambacho kitakuwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili, kiafya na kimaadili ambao ndio watakuwa wajenga hoja sahihi na makini katika ujenzi wa nchi.

Malezi yana mchango mkubwa katika jamii yetu kwa sababu ukiwa na kizazi bora chenye malezi mazuri kitaweza kuilinda amani tuliyonayo na kupaisha uchumi wetu kwa sababu ukishindwa kulinda kizazi hiki cha sasa hapo ndipo utakapo jenga jamii mfu isiyokuwa na maadili watu watatawaliwa na rushwa, unyang'anyi, unyanyasaji wa kijinsia na mengine mengi ambayo yataweza kusababisha maafa kwa baade hali inayoweza kuhatarisha usalama wa taifa mfano kukiwa na uongezeko la uhalifu itasababisha mgawanyiko na kuibuka kwa makundi mbalimbali ya ugaidi hali inayoweza kupelekea machafuko.
 
Upvote 4
Haya yote yanaanzia nyumbani.

Kabla ya kuwafikia watoto tuanze na wazazi. Hivi je wazazi wa kitanzania wanayafahamu malezi ya watoto.

Tunataka walezi bora, sio bora wazazi tu.

Hivi mleta mada unaonaje tukiajiri wanasosholojia na wanasaikolojia wa kutosha kufundisha wazazi kuwa walezi bora. Na iwe kanuni kwamba mzazi yeyote anapaswa kuonesha cheti cha kufaulu malezi ya mtoto ili aruhisiwe kuishi na mtoto wake. Kozi inatolewa hata wiki mbili tu kwa ajili ya ya msingi 'basics'.

Mzazi atakayeshindwa kusoma kozi hiyo kwa muda wake akiwa mjamzito, au mapema baada ya kujifungua anakabiliwa na kutenganishwa kwa muda na mtoto wake akalelewe na vituo vilivyotengwa na serikali vyenye wataalamu wa ulezi (sio uji wala mtama ULEZI/Malezi)wa watoto.

Mtoto atalelewa huko 'foster' homes hadi pale ambapo angalau mzazi mmoja atafaulu kozi ya malezi ya mwana . Ova.

Unalionaje hili, mleta mada?
 
Shida ilianza pale serikali ilipoanza kuingilia maswala ya familia kama kumuwezesha mwanamke na kupanga namna ya kulea watoto. Shida imeanza hapo.
 
Back
Top Bottom