Hakuna tofauti kati ya biashara na ajira

Hakuna tofauti kati ya biashara na ajira

Rog chimera

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
398
Reaction score
706
Salam wajomba na mashangazi,

Kumekuwa na tabia ya watu kutaka kuumwambfy ujasiriamali/biashara na kuufanya uonekane ni bora zaidi mara elfu moja ya ajira lakini ukichunguza kwa makini advantage iliopo katika ujasiriamali ni ndg sana.kivp? angalia hapa.

Ulinganishi wa juu
Wafanyabiashara wakubwa kama Mo na bakhresa hawawazidi sana wakurugenzi na mameneja wa makampuni makubwa na mabenki maana hawa huwa na hisa katka makampuni hayo na hupata mgao mkubwa sana ila tu sabab wao sio maarufu watu hawafahamu.

Kwaiyo kuwa mwajiriwa katk nafs za juu ya taasisi ni njia mojawapo ya kutajirika,usiseme ni ngumu kufika huko sabab kutajirika kama mo na bakhresa ni ngum zaidi.

Ulinganishi wa kati
Wafanyabiashara wenye kipato cha kati kwenye range ya 5,000,000 - 100,000,000 net profit kwa mwezi. Nao hawatofautiani sana na waajiriwa kwenye taasisi kubwa za binafsi.usiseme taasisi za binafsi ni wachache hata wafanyabiashara wanaopata hiyo faida kwa mwezi ni wachche mnoo na wanatumia mda mwingi na kazi ngum na uvumilivu kufikia hapo ukilinganisha na waajiriwa wanaopata kipato sawa na hicho kwa mwezi.

Ulinganishi wa chini
Kundi hili la wafanyabiashara wadg ndio liko hoi zaidi ukilinganisha na wenzao walioajiriwa , yani hawa wakiteleza kidg tu mtaji wte chali.wengi wao hupata wakati mgumu sana kukukza biashra zao na ni aslimia ndg kati yao hufanikiwa kupanda kwenda kundi la kati, pia hutumia muda mrefu sana ukilinganisha na wenzao walioajiriwa .

Ushauri wangu, usitishwe na habar za biashara.cha msingi tumia rasililimali ulizonazo kupata elimu hasa katika masuala ya sayansi na biashara .
Mfano mtu mwenye elimu ngazi ya shahada ya uzamili (masters)katika masuala ya engineering, medicine , law, finance ana nafsi kubwa ya kufanikiwa maisha kuliko mtu anaeanza biashara
No hard feelings, just common sense!.
 
Mkuu umejaribu kupita au kupata exposure kwenye makampuni binafsi?...

Tuanze na haya
1. Biashara kama Mo.entreprises hiwesi fananisha na mkurujenzi yoyote wa juu hata spate mshahara was bill 5 Kwa mwaka ,mfano MEtl INA revenue za bilioni 70 kwenye vinywaji tu na trilioni 2 Kwa ujumla .sasa assume Net Margin in 25% ? Mkurugenzi gani was juu anapata bil hata 10 mashahara?

-mkurugenzi anaelipwa sana mfano Kenya anapata tsh mil 200 Kwa mwezi late CEO wa safaricom

2. Ukizungumzia SMEs labda sanasana medium enterprises....ila large enterprises wapo watanzania wanazimiliki zikitengeneza faida bilioni hadi 10 Kwa mwaka

3.Unawajua watanzania wenyehisa nyingi kwenye mabenki?au taasisi kubwa hapa tanzania?.......
CEO wote mfano hapa tanzania share based compensations sijawahi ona kwenye large businesses anaemiliki hata 1% ,compensation ni ndogo sana ukilinganisha na dividends or residual /reserves
4.in general employees wanakula 10-20% ,shareholders they take it all

5.Biashara ni kaz pia kama kazi nyingime ,Luna wafanyabiasahra wadogo na wakubwa,pia kunawafanyakazi wadogo na wakubwa...............sio kila MTU anaweza Fanya Biashara,ila kama una passion na capability ,

Biashara it pays than salary ,sababu sekta binafsi ndio imeajiri sana kuliko hata serikali....sekta rasmi pia IPO mbele kwenye ajira ,ambapo Biashara zinamilikiwa na watu
 
Taja mfano wa bank au taasisi hapa tanzania inayotoa mshahara au total compensation ya bilioni 3 Kwa mwaka Kwa mkurugenzi

Tanzania bado sana.. waajiri wanabana sana wafanyakazi wao.. ghorofa za kariakoo za wakinga hata ajira wala shule hawazijui... mimi napoishi kila hotel kubwa au business kubwa ni ya mtu ambaye hajaajiriwa.
 
Wewe ni muoga wa Kutoka comfort zone endelea kuamka saa 12 kila siku katimize ndoto za wenzio..Wacha watu wajilipue maana wakifanikiwa watawasaidia watu wengine waoga Kama wewe kupata ajira..Jitahidi to convert your salary income to be passive income or portfolio income..
Bila shaka ww uko katika kundi la chini kabisa la wauza vibanda ndo maana umekuja na mihemko.
 
Bila shaka ww uko katika kundi la chini kabisa la wauza vibanda ndo maana umekuja na mihemko.
Wewe endelea kutimiza ndoto za wahindi na waharabu acha mimi niendelee na kibanda changu ili uyo mwanao atakapomaliza Elimu bure naye aje apate ajira I hope atanikuta nipo kwenye large enterprises..

Na kama akili zake mwanao ni kama zako awezi kupata kazi kwenye Hizo large private company na urithi pekee utakaomuachia ni title ya baba alikuwa mkurugenzi/manager/ kwenye shirik a fulan..
 
Rog chimera,

Ulinganishi wako asee sio relevant kabisa
Niliwai fanya kazi financial instituation flan na nlideal sana na mambo ya mikopo.

Nakupa mifano kwa vitendo
1. Nlikua nkishika salary slip za waajiriwa wengi wao wa serikali asilimia 99.5% hawakuwai fikisha Salary inayo zidi 5M per Month na kama walikuepo niwachache sana
Ambapo kuna wafanyabiashara wadogo tu wanapata zaidi ya iyo pesa na niweng sana mfano nina jamaa namfahamu yupo Mbagala anauza kuku wa kukaanga tena bloir kwa siku anauza sio chini ya kuku 70 na kwa mwezi asipo uza sana mauzo yakipungua anafunga na 2M as profit sio sale naomba uwelewe apo.

Kwa mauzo ayo just assume mtu ametoka chuo na degree yake unajua analipwa kima cha chini sh ngapi? Not more than 800K na unajua mpka afike kwenye 2M inahitajika effort gani? Inabidi ajiendeleze kitaaluma ( for instance 2 yrs ili awe na master degree ) mda huu mtu anasoma kubost mshahara wake na kupandishwa jua mwenye biashara atakua mbali

2. Wafanyakazi wengi wa serikali wanalipwa mishahara ya kipumbavu na si tu serikalin ata sector binafsi mfano unajua customer care wa voda na tigo wanalipwa sh ngapi not more than 450k pitisha apo income tax, Nssf , wengine loan board toa apo 15% na bima wanarudi nyumbani na 280k - 340k w
Je unajua kuna wamama uko mbande wanafuga kuku kwa mtaji wa 1.5M na wanapata faida ya almost 750k

Aya unajua mwalimu wa primary mwenye diploma analipwa sh ngapi 419,000 kama basic take home apo inaweza fika ata laki 280,000 jua akikopa apo atapokea 130,000 na kitu

Wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa unajua wanalipwa between 4-6M sema wanaposh na kwakua wapo kwenye system wanajua wanayoyafanya kupata pesa

Mfano mwingine

Najua unajua wakufunzi wengi wa vyuo vikuu wale maprofessor na madokta unajua wanalipwa kiasi gani ?
Haizidi 8M mkuu sema kinacho wabeba wanakua na posho na marupu rupu mengi na wanatengeneza pesa nyingi nje ya ajira mfano wanaandika ma proposal wanafundisha part time na mambo mengine je wametumia muda gani kuarchie ivyo vitu kama sio chini ya miaka 7-10 ila mfanyabiashara kwa muda uo atakua mbali sana.

Kuna kipindi nliwai shika salary slip ya daktari mmoja mpk anaenda staafu alikua ajagusa 5M

Uko mabank Unajua mateller wanapo anza wanalipwa kiasi gani ? Wengine mpaka 550,000 sema benefit wanazo pata ni bonus pamoja na loan za magari na nyumba zisizo na interest

Biashara inafaida zake na hasara zake lakini pia ajira inafaida zake na hasara japo
Ajira faida yake ni kua tu mtu anakua assured kila mwezi ata pokea fixed amount uki biashara mtu anaiaji ku struggle ili asishuahe mauzo

Ajira mtu anatumia salary kama collateral ya mkopo so anauwezo wa kujenga ila kwa biashara mtu kupata mkopo kwa biashara inayo anza ni ngumu na akipata ni mdogo

Ajira mtu anafaida ya Social security scheme baaada ya kustaafu ila kwa biashara hakuna labda kama alikua anafanya saving

Fatilia watu wengi walio staafu wakapata pesa zao asilimia kubwa awaendelei coz hawana elimu za biashara nje ya ajira zao

So naungana na mdau apo juu kuwa biashara inalipa sana kama ukiwa na nidhamu na ukijua unachofanya ila ajira ni utumwa uliokithiri na ulemavu wa kufikilisha ubongo
 
Kila kitu kinachangamoto zake hususani biashara inachangamoto kubwa Sana kulinganisha na ajira.

Cha msingi ni kustruggle upande wako ili kuongeza kipato kwa sababu kadili kipato kinavyo ongezeka ndivyo mahitaji na matumizi pia yanavyoongezeka.
 
Pia wafanyabiashara waliowengi wakubwa na waliofanya vizuri zaidi walipitia shule na walitoka kwenye ajira zenye maana,zaidi ya hapo basi ujue kanjubai katumika Sana.
 
Ndugu usifananishe kujiajiri na ajira...!!na ni wachache sana ambao hupata maendeleo kupitia ajira....!!

Aliyejiajiri ni boss mwenyew...!!hana mtu nyuma wa kumuamrisha...ana mteja mbele yake ambaye ana uamuzi wa kukubali au kukataa

Lkn pia maamuzi hufanya yeye mhusika na mtu mwngne...kuanzia bei...mda wa kufungua mpk cku ya mapumziko

Lakini pia aliyejiajiri anatafta future yake mwenyew na c ya mtu mwngne...!!daima kiu ya maendeleo humkuta mtu aliyejiajiri kuliko aliyeajiriwa...!!

Nakumbuka tlipokuwa field ndo nilijijua kuw kuajiriwa ni utumwa mno
Wahi saa 12
Hesab namba
Cmamia usafi
Ofisin unapanga timetable ya utachofundsha
Unamaliza cku nzima kzunguka darasa moja mpk jingne
Chakula mnakula sawa na wanafunz
Saa 8 wanfunz wanaondoka wew unabaki mpk saa 12

Just imagine hayo ndo maisha yako mpk ustaafu

Nilipostpone mwaka wa mwsho nkajpanga...nmfungua biashara...inanilipa na nnafurah nnachokifanya
 
Biashara daima itabaki kuwa bora kuliko ajira kama ikiendeshwa vizuri. Uchumi wa dunia hii unaendeshwa na kukuzwa na businesses ambazo kwa sehemu kubwa ni sekta binafsi.

Hata hao mabosi unaosema wanalipwa fedha nyingi nao wapo chini ya business ambazo wameajiriwa. Jiulize ikiwa hao waajiriwa wanalipwa fedha nyingi, je wamiliki wa biashara watakuwa na fedha kiasi gani?

Kitu ambacho unatakiwa kujua ni kuwa biashara inaweza kukua na kufikia thamani kubwa sana. Jambo ambalo ajira haiwezi kufanya, ongezeko la mshahara haliwezi linganishwa na business inayokuwa.

Wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara na wala wote hatuwezi kuwa wafanyakazi somewhere....we need each other. Ila siku zote mmiliki wa biashara ndiye anatake home a mammoth share.

Mwisho usiwadharau wafanyabiashara wadogo ukawaona wana hali duni sana. Hao mamantilie, wauza dagaa mitaani, na wengineo wengi wanawazidi kipato wafanyakazi wengi tu wa serikali au private.

Mimi kazi yangu ya kiprofessional imenikutanisha na wateja wengi wasio na elimu sana, wengine ni darasa la 7 tu...ila wana mafanikio ya kifedha makubwa sana ambayo kwa mtu anayetegemea ajira kama chanzo kikuu cha kipato kamwe hawezi kuyafikia. Usiidharau biashara mkuu.
 
Mara nyingi tunachanganya biashara, kazi na kujiajiri.

Iko hivi:
1. Mfanyakazi ni Mtu aliye ajiriwa au amejiajiri awe mchuuzi au mjasiriamali. Utakuwa mfanyakazi kama kipato chako kinategemea uwepo wako sehemu ya kazi.

2. Mfanyabiashara ni mtu ambaye amejenga taasisi ambayo mara nyingi ni kampuni, yenye mifumo na utaratibu rasmi wa uendeshaji wake. Hapa mwenye kampuni anaweza kupata faida hata kama hafanyi kazi. Kwa sababu kuna watu wanamfanyia kazi.

Tofauti na kazi, biashara inaingiza pesa hata bila mmiliki kuwepo au kuhusika. Mara nyingi mmiliki akishaweka mifumo madhubuti anakaa pembeni na ana oversee kwa juu pale na kuweka mikakati zaidi..

Biashara inaweza kurithishwa lakini lazi haiwezi kurithishwa. Ukiwa CEO wa kampuni kubwa hata kama unalipwa ma billion uki retire au kufa ndo mwisho wa mabilioni yako. Watoto au familia yako haiwezi kurithi kazi yako.

Utajiri unakuja pale ambapo mtu anakuwa na biashara (portifolio) zaidi ya moja. Umeshaweka mipango yako wewe unapata gawio tu, huku ukiendelea kula bata.

Infact mtoa mada ana point, kwa sababu watu wengi wanaojiita wafanyabiashara ni wafanyakazi waliojiajiri. Wabongo hatuna utamaduni wa kuweka mifumo na utaratibu wa usimamizi wa biashara zetu kiasi kwamba muhusika mkuu akiondoka na biashara inakufa.
 
Salam wajomba na mashangazi,

Kumekuwa na tabia ya watu kutaka kuumwambfy ujasiriamali/biashara na kuufanya uonekane ni bora zaidi mara elfu moja ya ajira lakini ukichunguza kwa makini advantage iliopo katika ujasiriamali ni ndg sana.kivp? angalia hapa.
Ulinganishi wa juu
Wafanyabiashara wakubwa kama Mo na bakhresa hawawazidi sana wakurugenzi na mameneja wa makampuni makubwa na mabenki maana hawa huwa na hisa katka makampuni hayo na hupata mgao mkubwa sana ila tu sabab wao sio maarufu watu hawafahamu.

Kwaiyo kuwa mwajiriwa katk nafs za juu ya taasisi ni njia mojawapo ya kutajirika,usiseme ni ngumu kufika huko sabab kutajirika kama mo na bakhresa ni ngum zaidi.

Ulinganishi wa kati
Wafanyabiashara wenye kipato cha kati kwenye range ya 5,000,000 - 100,000,000 net profit kwa mwezi. Nao hawatofautiani sana na waajiriwa kwenye taasisi kubwa za binafsi.usiseme taasisi za binafsi ni wachache hata wafanyabiashara wanaopata hiyo faida kwa mwezi ni wachche mnoo na wanatumia mda mwingi na kazi ngum na uvumilivu kufikia hapo ukilinganisha na waajiriwa wanaopata kipato sawa na hicho kwa mwezi.

Ulinganishi wa chini
Kundi hili la wafanyabiashara wadg ndio liko hoi zaidi ukilinganisha na wenzao walioajiriwa , yani hawa wakiteleza kidg tu mtaji wte chali.wengi wao hupata wakati mgumu sana kukukza biashra zao na ni aslimia ndg kati yao hufanikiwa kupanda kwenda kundi la kati, pia hutumia muda mrefu sana ukilinganisha na wenzao walioajiriwa .

Ushauri wangu, usitishwe na habar za biashara.cha msingi tumia rasililimali ulizonazo kupata elimu hasa katika masuala ya sayansi na biashara .
Mfano mtu mwenye elimu ngazi ya shahada ya uzamili (masters)katika masuala ya engineering, medicine , law, finance ana nafsi kubwa ya kufanikiwa maisha kuliko mtu anaeanza biashara
No hard feelings, just common sense!.
Nadhani umesahau kuwa biashara inakupa wigo mpana zaidi wa kupiga hatua kuliko ajira pia biashara inakupa security kubwa ya uchumi wako kuliko ajira nimekaa kwenye ajira miaka nane kwa makampuni manne tofauti na nimekaa kwenye ujasiriamali miaka sita nimeona tafauti kubwa mno. Naona biashara haihitaji uvivu ndio mana wengi wa naishindwa.

Ukiajiriwa unaweza usifanye ubunifu wowote na mzigo wako ukaupata kila mwisho wa mwezi kama kawaida ila biashara inakuchukua muda mwingi na akili sana kuendesha..hivyo kama hupendi kufikiri nje box usiingie kwenye biashara.
 
Back
Top Bottom