Hakuna tofauti kati ya wahubiri wakristo na motivational speakers wa duniani!

Hakuna tofauti kati ya wahubiri wakristo na motivational speakers wa duniani!

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Wengi wa hawa si wahubiri wa neno la Mungu wa kweli. Wataingiza tu maneno kama Yesu Kristo, Mungu Baba, Roho Mtakatifu, Biblia n.k kuwapumbaza watu ila uhalisia ni motivational speakers wanaotumia kichaka cha dini kutumia hamasa zao na kuchukua pesa za watu kwa jina la sadaka, matoleo,fungu la kumi, sadaka, maalumu n.k.

Nimeziomba sana mamlaka zilitupie jicho jambo hili. Tusiache watu wachache waliangamize taifa kwa kuharibu akili za watu kwa kisingizio cha imani. Hatua zisipochukuliwa matapeli wote watahamia huko maana huko wanapiga pesa kwa raha zao.

Hakuna bugudha. Ni kama kupata nchi unapoweza kuuza mihadarati hadharani ya kuharibu akili za taifa na hakuna anayekuuliza. Ninarudia tena mamlaka zisisubiri mpaka wasikie yale ya Kibwetere au au yale ya kule Kilifi ndipo hatua zichukuliwe.

Yale yote yalianza na mahubiri haya ya kuharibu akili za watu. Na was wawili husema MAJI YAKIMWAGIKA HAYAZOLEKI. Tusisubiri mpaka maji yamwagike.
 
Mm naunga mkono watu wanavyonyooshwa, yule kiboko wa wachawi namkubali sana naomba arudi nchini na raia tumsamehe aendelee na ibada 😎
 
Mm naunga mkono watu wanavyonyooshwa, yule kiboko wa wachawi namkubali sana naomba arudi nchini na raia tumsamehe aendelee na ibada 😎
Yule walimfukuza lakini cha ajabu wapo wengine tena redioni kabisa wanahubiri kwa style ile ile wanaachwa tu. Kwa nini??
 
Tuma sadaka ya kumshukuru Mungu kwa namba:0756789674.

JINA:BONIPHACE MWAMPOSA🤣🤣
Mataahira nadhani watatuma sana tu!!! Wakristo sijui akili tumeweka kabatini au wapi. Sielewi. Biblia yenyewe asilimia 90 hawaijui. Kutwa kucha kwenda kutafuta miujiza makanisani na kwenye makongamano. Mungu atatuadhibu maana tumekuwa kama yule mtumwa aliyepewa talanta akaenda kuifukia kwenye udongo badala ya kuitumia. Wenzetu talanta zao wanazitumia mpaka kutuletea vifaa tiba na kwenda mpaka anga za juu. Sisi za kwetu tumefukia kwenye udongo na kwenda makamisani kuomba miujiza!!!!
 
"eti manabii wana vyeti, kanisa lina account ya mitandao ya kijamii mpaka bank.
Wahubiri wanabishana kinguvu kanisa unajitangaza kutafuta umaarufu!"

DIZASTA VINA: KANISA
 
Kungekuwa na ukamilifu duniani kusingekuwa na haja ya YESU kuja duniani eti kuokoa, MUNGU aliona mapungufu, kwahiyo acha wajigaragaze tu fake haidumu, neno linasema Ufalme wa MUNGU utatekwa na wenye nguvu, sasa wewe legea utabaki na hao fake fake.
 
Kungekuwa na ukamilifu duniani kusingekuwa na haja ya YESU kuja duniani eti kuokoa, MUNGU aliona mapungufu, kwahiyo acha wajigaragaze tu fake haidumu, neno linasema Ufalme wa MUNGU utatekwa na wenye nguvu, sasa wewe legea utabaki hao fake fake.
Ubalikiwe sana kwa hii comment yako
 
Umetapeliwa nn, umeombwa nn, unaonaje uktupa suluhisho sasa maana kama ww jambo fulan halikusaidii unaona ni utapeli tu lakn kuna watu wenye pesa kuliko ww, elimu kuliko ww, matajiri, upeo kuliko nk wanaendelea nalo au wanaamin hcho usichokiamini sa tumuamin nani mkweli hapo ww au hao nliowasema hapo?
 
Utasikia ..."Mwakasege ndio mwalimu mkweli"...

Mtu anawajengea hofu...halafu anatengeneza mazingira kwamba kaiondoa hiyo hofu fake
 
Wengi wa hawa si wahubiri wa neno la Mungu wa kweli. Wataingiza tu maneno kama Yesu Kristo, Mungu Baba, Roho Mtakatifu, Biblia n.k kuwapumbaza watu ila uhalisia ni motivational speakers wanaotumia kichaka cha dini kutumia hamasa zao na kuchukua pesa za watu kwa jina la sadaka, matoleo,fungu la kumi, sadaka, maalumu n.k.

Nimeziomba sana mamlaka zilitupie jicho jambo hili. Tusiache watu wachache waliangamize taifa kwa kuharibu akili za watu kwa kisingizio cha imani. Hatua zisipochukuliwa matapeli wote watahamia huko maana huko wanapiga pesa kwa raha zao.

Hakuna bugudha. Ni kama kupata nchi unapoweza kuuza mihadarati hadharani ya kuharibu akili za taifa na hakuna anayekuuliza. Ninarudia tena mamlaka zisisubiri mpaka wasikie yale ya Kibwetere au au yale ya kule Kilifi ndipo hatua zichukuliwe.

Yale yote yalianza na mahubiri haya ya kuharibu akili za watu. Na was wawili husema MAJI YAKIMWAGIKA HAYAZOLEKI. Tusisubiri mpaka maji yamwagike.
Usichanganye samaki wazuri na waliooza kwenye kapu moja.

Ili twende pamoja, badili hiyo title uandike "Hakuna tofauti kati ya Wahubiri Wakristo wa Uongo na Motivational Speakers".

Biblia imeandika wazi kuna makristo wa uongo na manabii wa uongo na inatuonya tujihadhari nao.
Mt 24:24
"Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule."

Mathayo 7:15-29 BHN
“Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao."

Nakazia hapo: "Mtawatambua kwa matendo yao." Kama hujui jinsi ya kuwatambua manabii wa kweli na wa uongo, sema tukujuze.

Ukizuia Wakristo wa kweli kuhubiri Injili, tarajia ongezeko kubwa la wezi, majambazi, wanyang'anyi, waongo, mafisadi, mashoga, makahaba, wasiojali watu, wasiotenda haki, wanaojipenda wenyewe, wagomvi, wanaoonea wengine, wasio na huruma, wanaopenda rushwa nk nk. Jamii iliyojaa watu wa namna hiyo itakalika?
 
Yesu aligiza watu waambie kuwa Tubuni dhambi kwa maana Ufalme wa Mungu umekaribia. Ila haya mahubiri ya siku hizi ni namna ya kupata pesa. Shida ipo kwakweli.
 
Mataahira nadhani watatuma sana tu!!! Wakristo sijui akili tumeweka kabatini au wapi. Sielewi. Biblia yenyewe asilimia 90 hawaijui. Kutwa kucha kwenda kutafuta miujiza makanisani na kwenye makongamano. Mungu atatuadhibu maana tumekuwa kama yule mtumwa aliyepewa talanta akaenda kuifukia kwenye udongo badala ya kuitumia. Wenzetu talanta zao wanazitumia mpaka kutuletea vifaa tiba na kwenda mpaka anga za juu. Sisi za kwetu tumefukia kwenye udongo na kwenda makamisani kuomba miujiza!!!!
Kusema ukweli Waafrika tuna safari ndefu sana.Sijui ni uwezo wa watu kufikiri upo chini sana?Yaan nikianzisha dhehebu kwa kujipanga vizuri mwaka mmoja nitakuwa mtu maarufu sana.
 
Back
Top Bottom