Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HAKUNA TUMAINI MBELE; TUMAINI TUMELIACHA NYUMA.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel.
Mambo yataendelea kuwa vivi hivi. Tena yatazidi kuwa magumu, kila siku iendayo na ile inayokuja itakuja na ugumu maradufu. Hakutakuwa na urahisi. Watu watazidi kuchanganywa na kujichanganya. Furaha itazidi kuyoyoma na moyo kupogoma.
Hakuna TUMAINI KESHO, tumaini tuliliacha nyuma.
Tumaini la maisha mazuri tulishalipita miaka kadhaa iliyopita, tumaini la furaha katika ndoa zetu tulishalipuuza na sasa tumechochola katika vichochoro vyenye giza na ukungu upofushayo macho yetu, Loooh! Tumekuwa vipofu hata hatuioni njia tuiendeayo, tena hata ile tuliyoijia tumeisahau. Ole wetu sisi kwa maana Tumaini tumelipa mgongo, nasi tunaiendea taabu na huzuni.
Wengi pengine hujipa moyo, husema KESHO YAO ITAKUWA NZURI KULIKO LEO, wengi wengine hudanganywa huko mimbarani na makuhani na maimamu, tena majukwaani waliko siasani hao viongozi huwapa maneno mazuri wakisema; Kesho yetu! Kesho njema inakuja. Tujipe moyo, Taifa letu litakuwa bora, na maisha yetu yatastawi na kila mmoja wetu ataifurahia nchi hii, kesho! Kesho yenye matumaini"
Hivyo ndivyo wasemavyo hao wenye kusimama mdomo ukiwa wazi, wapigao kelele sizizo na nguvu, wapigao hatua zisizo na mwendo. Looh! Wasijue tumaini halipo tena na Faraja tulishaipuuza.
Hakuna maisha mazuri tena huko mbeleni, maisha mazuri tulishayaacha nyuma.
Ima turudi nyuma tuifuate njia kuu, lilipo tumaini ama tuendelee kusonga mbele kuliko na giza na maumivu.
Siwakatishi tamaa isipokuwa naongea iliyoamini, mbele hakuna tumaini, mambo yatazidi kuwa magumu tena magumu hasa.
Tumeacha Tumaini katika njia kuu za msingi.
Vijana wanasubiri maisha mazuri, hilo ndio tumaini lao, wamekaa kitako hawataki kufanya kazi zenye matumaini, wao husubiri matumaini ya wageni, tena wageni kutika nchi za mbali, nchi za barafu. Looh! Enyi zirudieni kazi za Babu zenu, mkazifanye kwa maana huko ndiko liliko tumaini, lakini ninyi mmesema HAMTAKI Kuzirudia kazi za Babu zenu. Haya sasa subirini muone, hali yenu na hali za Babu zenu ipi itakuwa bora.
VIJANA wanasubiri NDOA zenye waume na wake wazuri. Wamekaa kitako vijiweni na huko mitandaoni. Tena wanawake husubiri waume wenye Pesa, wakati huo huo Vijana wakiume nao wanatafuta wanawake wenye pesa na wazuri, wakifikiri hilo ndio tumaini ndani ya ndoa litakalowapa furaha. Umri wao unasonga, miaka ya kuoa na kuolewa inapita, ngozi zao zinalegea na sauti zao zinakuwa nzito; hayo hawayaoni kuwa ni dalili kuwa huko mbele hakuna tumaini, wao wanasema umri wa kuoa au kuolewa Bado, tena husema hakuna umri wa kuoa au kuolewa. Loooh! Haya nayo yanasikitisha katika zama hizi.
Tazameni nyuma Babu zenu walifanyaje, lakini ninyi mnasema, HATUTAKI kutazama mambo ya Babu zetu. Nanyi hamkujua yajayo kesho ndio haya haya ya leo na yale ya jana na juzi, wala hapa mambo mapya katika dunia hii. Lakini ninyi mnataka kuvumbua mambo yenu. LOOH!.
Wanawake nao wanataka HAKI SAWA hilo ndilo kwao huliona kama tumaini jipya, Wasijue kuwa tumaini waliliacha nyuma yao. Wao hutaka uhuru ambao ni hakika hautawasaidia isipokuwa utazidi kuwaumiza na kuwadhalilisha mpaka watakapozirudia njia za zamani. Lakini wao husema HATUTAKI kuzirudia njia za zamani, sisi tunataka haki na uhuru kama walivyo wanaume. Tunataka tuwe wanaume na wanaume wawe wanawake. Looh! Basi hakuna tumaini lenu huko mbele, mtalia wala hamtanyamaza, mtadhalilika wala aibu yenu haitaondoka. Mama na mtoto watalala na Mwanaume mmoja kitanda kimoja, tena mtoto atazaa na Mama yake, na binti atazaa na Baba yake. Tena haitakuwa ajabu kuona nyuchi za wanawake barabarani kama wanyama waporini. Hivyo ndivyo mlivyotaka, na ndivyo itakavyokuwa. Sasa mtasema hilo ndilo lilikuwa tumaini lenu au tumaini lenu mliliacha siku za nyuma?
Nao wanaume wameacha asili yao, siku hizi wamekuwa kama wanawake, hilo kwao ndio wameliona ndilo tumaini pekee la kulifuata. Kiasili mwanamke hufanya vitu kumridhisha na kumfurahisha Mwanaume. Mwanamke hujiremba ili amfurahishe mume au wanaume, mwanamke hujikoga na kuleta maringo kumpagawisha mwanaume, mwanamke huichagiza sauti yake kumzuzua mwanaume lakini zama hizi mambo yamebadilika. Zamani ilikuwa jukumu la mwanaume ni kuitunza na kuilinda familia, hayo ndio majukumu makuu ya mwanaume. Lakini siku hizi wanaume ndio wanataka kumridhisha na kumfurahisha mwanamke, wasijue kuwa mwanamke hajaumbwa kuridhika wala kufurahishwa kwa maana yeye mwenyewe ni furaha. Mwanamke hajaumbwa kuchekeshwa kwa maana yeye mwenyewe ni kicheko, isipokuwa ameumbwa KUTUNZWA NA KULINDWA. Sasa wanaume kujiremba kama wanawake imekuwaje tena, kuzichombeza sauti zenu kama majike ati muwazuzue wanawake imekuwaje tena, kutengeneza shepu zenu ili mpendwe na kinadada imekuwaje tena, kunywa madawa ya nguvu za kiume imekuwaje tena? Tambueni hilo sio tumaini bali mnajiumiza tuu na kujigeuza wanawake. Lakini ninyi mkasema HATUTAKI kuwa wanaume tunataka kuwa kama wanawake. Haya msiwalaumu wanawake watakapowazingueni.
Tambueni mwanamke ukishashindwa KUMTUNZA na KUMLINDA huna utakalomfanyia akakuona wewe ni mwanaume, isipokuwa atakuona wewe ni mtumwa wake tuu.
Hakuna tumaini mbele ndugu zangu, tumaini tumeliacha nyuma.
Kama alivyosema Yeremia 6:16
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Simameni katika njia panda, mtazame. Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani. Tafuteni mahali ilipo njia nzuri muifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu. Lakini wao wakasema: ‘Hatutafuata njia hiyo.’
Kiswahili cha kizamani
Yeremia 6: 16
BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo"
Usijipe moyo, huko mbele hakuna Njia, hakuna Tumaini. Tazama walivyofanya zamani wakaishi kwa amani.
Maisha hayatakuzingua
Ndoa haitakuzingua
Kazi hazitakuzingua
Kila kitu kitaenda sawa.
Sio ujipe Moyo kuwa ipo siku, hakuna siku hiyo, acha kujiongopea.
Ulikuwa nami mwana wa TIBELI nyota ing'aayo yenye mbawa mbili irukayo ulimwengu huu na ulimwengu mwingine.
Nikupongeze kwa kusoma mpaka hapa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Chalinze, Pwani