Hakuna uchawi wa chuma ulete, ni visingizio vya watu wazembe

Chuma ulete ipo ishawahi kutokea dada mmoja alikuwa mate wetu chuo. Siku hiyo alienda mjini kununua mahitaji,,akaenda benki akatoa na fedha kiasi cha laki 6 ili alipie ada. Kufika kwenye daladala akatokea mtu mmoja akamwambia dada naomba unisaidie chenchi akatoa naote ya elfu kumi mdada akampa elfu 5 mbili ambapo ile elfu kumi akaiweka kwenye zile hela zingine. Kufika rumi fedha zote hazipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu kama hicho, Kuna muda uliacha wazi akachukuwa mtu
 
Elimu nzuri sana umenipa mdau,ubarikiwe sana kwa kutokuwa mchoyo wa madesa.😁🤣🤣🤣💯💯
 
Uchawi ni imani ya kijinga tu, kuamini vitu ambavyo havina uhalisia.

Na imani hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na imani nyingine za kijinga, kama dini, mizimu etc.

Nje ya hizo imani za kijinga, hakuna uchawi.
 
Ila huenda una kamzizi ka siri. Mf. Jamaa wawili wanalima eka Moja zilizopakana, ardhi ni ileile na kila mtu anatumia utaalamu wa kilimo. Juhudi zao zinafanana ila mmoja alivuna gunia 5 na mwingine gunia 1. Ujue Kuna chuma ulete ya shamba,sembuse biashara. Wewe sema haya mambo yapo subiri yakupate ili uamini.
 
Uchaw upo taikon mimi nilipigwa 500k kimazingira yakikukuta hautaaandika tena ulichoandika.

Nilipewa 500k nikaweka kwenye droo na sijatoka ndani na hajaingia mtu hiyo pesa sikuiona milele na sitoiona tena
 
chuma ulete ipo, ni imani iliyopo ndani ya vichwa vya watu ambao wamelelewa kwenye kuamini ushirikina,haijalishi elimu yako au imani ya dini uliyonayo,na imani hiyo ndio inayowafanya watoe ushuhuda ambao sio rahisi kuuthibitisha kwasababu wewe unaepewa ushuhuda huo hukuwepo
 
Pengine huwezi ukawa unaamini ushirikina ikiwa umekulia sehemu ambayo watu hawajihusishi sana na huo ushirikina, tatizo pia kwamba ni rahisi kuukataa uchawi.
 
Vizuri sana, me mtaji wangu nliupata kupitia boom...na baadae nkapewa support kidogo [emoji120]
 
Ñi kweli kabisa uchawi ni imani na mindset ya mtu ndio maana Kuna msemo maarufu "ALIWAZALO MJINGA NDIO LITAKALOMTOKEA"
 
Alafu unakuta kijana kabisa anaamini kuna watu wanavuta hela.
 
Kua na tembea ujionee mengi ya Dunia kwa ulivyotiririka hapo inaonyesha wazi kwamba kwanza ni mdogo kiumri na pili hujatembea kwenye jamii mbalimbali.
Onyo
Hii mentality yako iishie humu humu kwenye mitandao mana ukiipeleka mtaani watakutest na cha 150 tu, ukaiaga dunia kabisa.
 

Ni umri gani mtu akifika ndio atajua hayo mambo na kuyaamini na kuyatumikia?

Mimi nimeongea kulingana na utafiti niliofanya. Wewe unaongea habari za vijiweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…