Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,317
- 1,320
Habari Wana jf
Kama katiba ni Ile Ile,
Msajili wa vyama vya siasa ni yule yule,
Tume ya uchaguzi ni Ile Ile, matokeo ya uraisi hayahojiwi popote baada ya kutangazwa.
Wasimamizi wa uchaguzi ni wale wale, TAMISEMI na WAALIMU.
Sheria za uchaguzi ni zile zile,
Jeshi LA polisi ni lile lile La kukimbia na mabox ya kura,
Mahakama ni zile zile,
Ccm ni Ile Ile isiyokuwa tayari kuachia madaraka Kwa njia ya uchaguzi,
Dola ni Ile Ile ya kutumiwa na ccm Ili ibaki madarakani.
Unyama, vipigo, mateso utekaji na kusulubiwa Kwa wapinzani hasa chadema kupo pale pale.
Kwa kweli kwenda kwenye uchaguzi ni kupeleka vijana na wanachama wetu machinjioni.
Tubadili mbinu za kupambana na ccm, tutumie hizi hizi wanazotumia wao.
Tusimwachie Mungu mambo/ wajibu tunaopaswa sisi kuutimiza.
Siasa za tanzania Kwa Sasa zinatakiwa ziwe jino Kwa jino,jicho Kwa jicho ukipigwa jicho piga sikio tofauti na hivyon ni kujilisha upepo na ccm itabaki madarakani miaka 1000.
Tumaini la wapiga kura hasa wa upinzani ni kuona upinzani usiokubali kuibiwa, kuonewa, kutekwa, n.k
Bila upinzani imara na mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi hatuna haja ya uchaguzi maana ni kuhalalisha wizi na dhulma za ccm.