Hakuna USAWA WA KIJINSIA pasipo kwanza kuwa na USAWIA WA KIJINSIA

Hakuna USAWA WA KIJINSIA pasipo kwanza kuwa na USAWIA WA KIJINSIA

G-Mdadisi

Senior Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
165
Reaction score
100
#GMdadisi

Wengi tunachanganya na kujikuta tukipotosha zaidi kuhusu dhana ya usawa wa kijinsia kwa kutokujua vizuri.

Bahati mbaya sana wengi wameaminishwa na wanaamini Usawa wa kijinsia (gender equality) inawahusu zaidi wanawake kuliko kundi lingine.

Kuna USAWA WA KIJINSIA (Gender Equality) na kuna USAWIA WA KIJINSIA (Gender Equity) vyote vinafanya kazi pamoja.

Unapozungumzia USAWA WA KIJINSIA unagusa kumpa mtu kitu/fursa bila kujali ni mwanamke, mwanaume, mtoto, mlemavu, mzungu, muha au tajiri ilimradi wote wataanza kwenye msitari mmoja.

Mfano: Mwalimu anapotoa adhabu kwa wanafunzi darasani kwa kosa la kuchelewa kuingia darasani (viboko 6 kila mmoja) anatakiwa (agawe wastani kwa idadi 🤣) wote wachapwe sawa sawa bila kujali huyu ni msichana, ni mlemavu au sababu yoyote ile. HUU NDIO USAWA WA KIJINSIA.

USAWIA WA KIJINSIA inahusisha kuweka mazingira wezeshi kwa makundi yote kupata na kuzifikia fursa kwa pamoja bila kujali changamoto zao.

Mfano. Mwalimu anapotaka kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa kosa la kuchelewa darasani, anapaswa kwanza kuhakikisha kutazama kama wanafunzi wote wana mazingira sawa ya kuwawezesha kuwahi darasani kwa muda. Mfano ulemavu au umbali. Huwezi kutaka mlemavu awahi darasani wakati hana zana za kumwezesha kuwahi, hivyo lazima kwanza wawezeshwe ndipo waadhibiwe sawia.

Hakuna USAWA WA KIJINSIA pasipo kwanza na USAWIA WA KIJINSIA

#GenderEquality
 
Hapo ndio kuna tatizo hapawezi kuwa na equality kwa sababu jinsia zipo tofuati , lazima wapewe mahitaji kulingana na mahitaji yao ili wote wafikie malengo (Equity)
 
Back
Top Bottom