Inatakiwa kupunguza matumizi kwa kiasi kukubwa ili kipato kifanane na matumizi, ukiangalia hata katika ngazi ya familia huwezi kutumia zaidi ya kipato chako. Kiongozi anatakiwa ajiamini na ahakikishe kuwa anatafuta namna nzuri ya nchi kujitegemea. Utawala mbovu (kushindwa kujitawala) hasa kwenye usimamizi wa raslimali za nchi ni tatizo sugu kwahiyo nitajaribu kuelezea ni kwa kiwango gani uzalendo unavoweza kutusaidia kutunga sheria na kusimamia kipato cha nchi ili kuikomboa nchi kutoka kwenye umasikini, ujinga, ufisadi, rushwa, na matatizo lukuki yanayotukabili ambayo ndio chanzo kikubwa cha kuto kufanikiwa kwa nchi yetu.
UZALENDO NA USHIRIKIANO
Nchi nyingi zilizofanikiwa walitumia nguvu kubwa sana, kama marekani na uchina walitawaliwa pia lakini walipoamua kuweka siasa kando na kufanya kazi kwaajili ya nchi walifanikiwa. Mafanikio ya nchi ni uzalendo wa kuipambania nchi, vijana wengi tumepandikizwa uoga na hatuna uzalendo.
Viongozi waliotuhangaikia mpaka kupata uhuru wangekuwa waoga na kujipendekeza mpaka leo tungekuwa chini ya ukoloni, walijitoa kwa dhati wengine walikua tayari hata kufa ili wapate uhuru.
Sasa hivi tunatawaliwa na viongozi wetu ambao ni sisi tumewapa mamlaka tunawaogopa na wengi wetu tunasingizia familia au kuwa tumetingwa sana na shughuli zetu hatuwezi kuwa na shughuli huku tumetawaliwa tubadirike ndugu zangu uoga hauta kufikisha popote zaidi ya kuendelea kuwa masikini wa fikra na umasikini kiuchumi.
Mapolisi, Madaktari, Waalimu, Mameneja na nafasi yoyote ile serikalini jaribu kuionea huruma nchi yako acha rushwa, ubadhirifu wa fedha, kuwaonea watu wanaodai haki zao usifanye kazi kwa shinikizo lolote ila fanya kwa uwajibikaji na kufuata haki.
Kufanya kazi kwa bidii sio tu kazi za ofisi hata nje ya ofisi, acha kufanya kazi kwa njaa njaa zako tubadilike, njaa haziwezi kuisha kamwe kwa kufanya kazi kwa kuwaogopa viongozi wetu au kwa kutapanya mali za uma tufanye kazi kwa bidii.
Umasikini wa nchi yetu tumeutaka wenyewe kwasababu tumekosa uzalendo na hatuna ushirikiano. "Tusiiulize serikali yetu imetufanyia nini tujiulize kila mmoja kwa nafasi yake ameifanyia nn serikali yake?" Kila mmoja wetu anayo nafasi fulani ya kulifanya taifa hili liwe masikini au taifa lenye mafanikio hili litawezekana kwa kiasi kikubwa sana kama tu tutajua namna nzuri kwanza ya kuwapata viongozi wazuri na kama kiongozi akishindwa kutufanyia kazi tuwe na namna ya kumuondoa au ya kumuwajibisha kwa wakati tusiwape mamlaka kubwa sana viongozi wetu. Hatuna ule pia kuunda umoja wa kutufanya tukaungana kukataa au tukaunga mkono jambo fulani,
Vijana tufanyeni kazi kwa bidii nikweli hakuna ajira lakini sio kwamba ukijitahidi huwezi kufanikiwa haijalishi umesomea nini au umesoma kiasi gani ukitafta utapata tu ni bidii yako na kama tutafanya kazi itatuepusha na kujipendekeza, tunajipendekeza mnoo kwa watu wenye mamlaka mpaka inatia aibu mtu umesoma kabisa na elimu yako lakini unakaa kusifia sifia tu huoni madhaifu kabisa hata ukiona unakuwa huwezi kuyasema ili upate kacheo flani ni aibu ni aibu kubwa sana usomi sio kujipendekeza tubadirike ndugu zangu sijakataza kusifia ukisifia sifia lakini na penye madhaifu sema ukweli tusifate mkumbo ukielimika maana yake wewe ni kiongozi jamii inakuangalia.
MAMBO YANAYOTAKIWA KUFANYIWA MABORESHO YA HARAKA.
Mabadiliko makubwa yaanzie Kubadilisha katiba, katiba iliyopo nchini imepitwa na wakati yapo mambo ya msingi mengi ya kuyatoa na kuongeza mapya, ukitaka kuijua kesho ya nchi anzia kuangalia katoba yake.
Kupunguza matumizi makubwa ya sasa hasa yasiyo ya msingi mfano, ulipaji wa mishahara mikubwa kwa hizi nchi zinazoendelea inapaswa kuwa kosa kisheria kujilipa au kupandisha mshahara kuwa mkubwa kuwe na mshahara wa wastani. Kupandisha misharara kunatakiwa kuendane na kasi ya ukuaji wa maendeleo ya nchi kiuchumi.
Usitishwaji wa ununuzi wa magari ya serikali usio na ulazima hasa haya ya gharama kubwa, miaka ya leo nikawaida kuona magari ya kisasa tena yenye matumizi makubwa ya mafuta mengi sana kwamfano katika ofisi za serikali, matumizi haya makubwa yanatudidimizi.
Serikali haitakiwi kumsomesha mtumishi yeyote haya ni matumizi mabaya ya fedha za uma kama mtumishi hajakidhi vigezo au elimu yake ni ndogo anapaswa kujiendeleza kwa nguvu zake mwenyewe. serikali itafanya kazi moja tu kumtunzia nafasi yake serikali ya sasa inamsomesha mtu na inaendelea kumlipa mshahara sidhani kama ni sawa.
Serikali haipaswi kulipa malipo ya awali kwa mfanyakazi haya huwa yanatolewa mtu anapopata tu kazi mtu akipata kazi anatakiwa aende kazini na mshahara ataukuta uko tayari kulipwa malipo ya ela ya kufikia kazini au yakuanzia maisha ni kulirudisha nyuma taifa hii haina umuhimu.
Serikali haipaswi kumlipa mstaafu hela ya kurudi kwao/kumsafirisha
Kupunguza manunuzi ya nguo kutoka nje tunapaswa kushindana na mataifa mengine hasa kwenye swala la mavazi na urembo tunapaswa kupunguza manunuzi ya nje kwenye nguo na urembo hasa kwa kuongeza kodi katika bidhaa za nje zisizo na ubora mfano nguo zilizotumika.
Itaftwe namna ya kuwasaidia wahitimu vijana ndo taifa la leo ikiwa vijana watakaa kusubiri kazi taifa haliwezi kufanikiwa vijana wakiwa zaidi tutakua tunaandaa vijana wa kujipendekeza ni rahisi taifa kufanikiwa wafundishwe ni kwanamna gani wanapaswa kuwa wabunifu na wao ndo wanategemewa hvyo wanatakiwa kujitoa kweli kweli.
Haitakiwi serikali imsafirishe mfanyakazi anapoenda kazini mfanyakazi wa serikali anapaswa kutumia usafiri wa kawaida wa uma au binafsi na sio kununuliwa gari na serikali, kama mfanyakazi atakuwa na gari ya ofisi itakuwa ni kwaajili ya kazi za kiserikali tu na sio matumizi binafsi (tunahtaji kujitoa kwaajili ya taifa letu na sio kulinyonya taifa)
Kufuta kabisa misafara ya viongozi kiongozi anapaswa kusafiri bila msafara usio na maana
Kufuta sherehe za Kiserikali zisizo na umuhimu kama vile sherehe za uhuru tunatakiwa kujua kuwa uhuru ni mafanikio kiuchumu na sio sherehe.
Kuhamasisha teknolojia za ndani zipo teknolojia nyingi sana ambazo zikipata mkono wa serikali kiuchumi ni mafanikio makubwa sana katika nchi
Kuunda jeshi lenye maono ya teknolojia tunapaswa kupunguza manunuzi ya seraha kutoka nje tunapaswa kutengeneza wenyewe hasa zinazoendana na mahitaji ya sasa.
Kuboresha kilimo kwa kuwasaidia wakulima serikali inapaswa kuongeza nguvu kubwa kuwasaidia wakulima na hii inatakiwa iegemee kwenye ubunifu wa teknolojia ya madawa na zana za kilimo na sio kutegemea kila siku kununua kutoka nje ya nchi kwa kutumia taasisi ya utafiti wa kilimo TARI serikali inatakiwa ifanye utafiti wa kina na kuja na majibu yanayoeleweka ni kwavipi tunaweza kumuinua mkulima na kubadirisha dhana ya kilimo kuonekana kama kazi ya mtu alieshindwa na kuwa njia kubwa ya kujiajiri na kupata mafanikio ya kweli.
kuboresha namna ya usimamizi wa miradi pesa nyingi sana zimekuwa zikipotea kwenye miradi ya maendeleo hii ni kutokana na usimamizi mbovu na wananchi kukosa uzalendo
Taasisi za uma hazitakiwi kufanya kazi kwa hasara bila sababu zisizo eleweka, Taasisi inatakiwa kupewa vigezo na mashariti ambayo wasipofata watawajibishwa na pia inatakiwa wataalamu wa taasisi wafanye tathmini na kutoa mapendekezo ya muhimu kuondokana na hasara yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka.
Na kwakumalizia kila mtu awajibike jwa nafasi yake kadri awezavyo tuondokane na hali mbaya tuliyonayo

Upvote
1