Hakuna uzito wa mashairi kama yangu uliotokea katika taifa hili – Afande Sele

Hakuna uzito wa mashairi kama yangu uliotokea katika taifa hili – Afande Sele

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii Mkongwe wa Bongo Flava, Afande amefunguka sababu ya kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma mpya.

Mkali huyo wa rhymes ameiambia Planet Bongo ya EA Radio yupo mbioni kutoa ngoma mpya kwani watu wake wanamuulizia sana kutokana na uzito wa mashairi yake.

“Mimi nina nyimbo nyingi zilizo bora isipokuwa nawaomba wanipe muda nafaikiri kabla ya Pasaka nitatoa wimbo mpya kwa ajili yao kwa sababu maombi yamekuwa mengi na nidhani wamekosa mawazo yangu na hakuna uzito wa mashairi kama yangu uliotokea katika taifa hili,” amesema Afande Sele.

Ameongeza kuwa muziki umekosa mtu wa aina yake na kilichomkimbiza katika game ni kushauriwa kufanya muziki wenye swag ambao yeye hauwezi.

Ngoma ya mwisho Afande Sele kutoa na kufanya vizuri inakwenda kwa jina Dini Tumeletewa ambayo alimshirikisha Belle 9.



Bongo 5
 
Tatizo la huyu jamaa ni kujifanya anajua kila kitu wakati hana tofauti na Mrisho Mpoto
 
Na profesa J mbunge wa mikumi asemeje sasa. Yeye aseme tu ashachoka na apumzike tu na wajukuu zake.
 
Back
Top Bottom