Ntaganda boy
Member
- Jan 16, 2016
- 90
- 59
Wakati tuko kwenye wimbi kubwa la watanzania na dunia nzima kuathiliwa na magonjwa na changamoto za kisaikolojia au magonjwa ya Akili, bado serikali ya Tanzania haijatengeneza miundombinu ya watanzania kuwa na uwezekano wa kupata huduma na kuwepo na huduma zenyewe.
Hadi sasa idadi ya wagonjwa ni zaidi ya Bilioni moja na hii ni kutoka watu milioni 900 iliyokadiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)kabla ya janga la Korona na mwaka 2022 kutoa taarifa ya kuogezeka kwa robo nzima maana kutoka milioni 900 hafi kufikia bilioni 1 na milioni 200.
Dunia ya nchi zilizoendelea tayari zilishatengeneza miundombinu ya wananchi wake kupata huduma lakini pia kwa Tanzania, upande wa Zanzibar tayari wao walishaweka wazi kwa wananchi kupata huduma za Afya ya Akili na Saikolojia maana miundombinu yao na rasilimali iko wazi maana wao wanatoa ajira kabisa kwa wataaluma wa Afya ya Akili na Wanadaikolojia na inatambulika kama ajira rasmi.
Kuna sababu kadhaa zinazoonyesha kuwa Wizara ya Afya na TAMISEMI kulitilia jambo hili mkazo na kulipatia nafasi ili jamii nayo ifaidike na huduma za kisaikolojia au Afya ya Akili.
Hadi sasa jamii huwa inaamshwa na kukumbushwa kuwa kuna swala la Afya ya Akili baada ya kutokea matukio ya watu kujiondoa uhai wenyewe hasa katika Jiji la Dar Es Salaam zaidi lakini pia tukumbuke kuwa kuna vitendo vya ukatili vyenye mahusiano na Afya ya Akili hasa kwa kuangalia takwimu kadhaa kama vile;
2021 pekee vifo zaidi 470 vya Watanzania chanzo chake ni ukatili na kujuondoa uhai, taarifa waliyochapisha LHRC May 31 2022.
Kuna vitendo zaidi ya 42,414 vya ukatili kwa mwaka 2021. Kumaanisha kuna ongezeko la idadi ya watu na Watoto wanaofanyiwa ukatili kwani kwa mwaka 2020 visa vya ukatili vilikua takriban 30,000.
Tukumbuke si wanawake wala Watoto tu wanaofanyiwa ukatili pekee bali na wanaume japokuwa ukimya katika kutoa taarifa ndio huficha Habari zao na laiti wanaume wakianza kutoa taarifa basi idadi ingekuwa maradufu.
Kuanzia Januari 2022 hadi Julai 2022, kuna zaidi ya matukio 100 yaliripotiwa na vyombo vya habari juu ya kuuana au kujiua. Kuna mikoa ilitajwa kama kinara katika Habari hizo, mfano Mwanza, Geita, Iringa, Dar es salaam na hivi karibuni imeripotiwa Kigoma kwa tukio la familia moja kuuliwa na Dodoma kwa visa vya mapenzi.
Kwenye vyombo vya Habari hasa Habari za mauaji Jiji la Mwanza na Mkoa wa Geita ni vinara kusikika, hali hii inazua taharuki kwa wakazi wa mikoa hiyo lakini zaidi kwa wageni ambao wanaamini kuwa wakazi wa mikoa hiyo ni wakarimu Zaidi.
Je mwaka 2023 ni sehemu ipi imetikisa na kusemwa
Mkoa wa Arusha ni moja ya kielelezo juu ya kuongezeka kwa wahitaji wa huduma za kisaikolojia, kulingana na taalifa iliyotolewa na Hospitali ya KCMC tarehe 04/06/2023 na kuchapishwa na magazeti juu ya Kanda ya Kaskazini wagonjwa wa Afya ya Akili kuongezeka na kuongeza siku za kupata huduma ndani ya wiki.
Hii ni kanda moja na hapa bado haijaingia Kanda ya Kati, Kusini, Magharibi, Kanda ya Maziwaa makuu, Pwani na Mashariki.
Hali ya Huduma Nchini Ikoje
Hadi sasa hospitali zinazotoa huduma za Afya ya Akili ni Hospitali za Rufaa zaidi na kadhaa za mikoa, pamoja na kutoa huduma lakini bado zimejaa na changamoto za kukosa watoa huduma hizo maana utakuta hospitali moja ina Psychiatric mmoja na hiyo ni hospitali ya Rufaa au Kanda. Hospitali hiyo haina Mwanasaikolojia au Mnasihi hata mmoja na hii haijalishi ukubwa wa hospitali na idadi kubwa ya wagonjwa wanaokuwa nao.
Hadi sasa serikali kupitia Wizara ya Afya na TAMISEMI bado hazijatoa nafasi kwa wanasaikolojia na wanasihi maana hakuna ajira yotote kuwahusu wao na hakuna aliyeajiliwa kwa taaluma hiyo na kutumia nafasi ya jina hilo (Tittle) na wanaofanya kazi kama wanasaikolojia ni madaktari walioenda kuongeza elimu na kuwa Psychiatrist na hawa hutoa huduma za dawa zaidi na si tiba za kisaikolojia saidizi mfano tiba maongezi na zingine sambamba za kisaikolojia.
Kitu cha Kufanywa na Wizara ya Afya na TAMISEMI
Ni juzi tu ya tarehe 05/06/2023 TAMISEMI ilitema mamia ya ajira za Afya lakini hakuna Mwanasaikolojia na Mnasihi hata mmoja na wakati huo Wizara ya Afya katika vipaumbele vyake vya Afya, Afya ya Akili iko katika nafasi ya sita ila watoa huduma wake hawapo kabisa katika mpango wa kuajiliwa na kupewa hizo nafasi za kuihudumia jamii.
Hadi sasa vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na baadhi za Mikoa hazina watoa huduma wa Afya ya Akili na Wanasaikolojia. Ukweli ni kuwa Muhimbili ambayo ndio hospitali ya Taifa bado pia haina wanasaikolojia na wanasihi wa kutoa tiba maongezi.
Kigezo tu cha kujitolea kama Mwanasaikolojia na Mnasihi katika Idara ya Afya ya Akili ni hadi uwe na Shahada ya pili na iwe Saikolojia Tiba tu (Clinical Psychology Only) wakati huo Tanzania ina maelfu ya wanasaikolojia na wanasihi wenye Shahada na Stashahada wa kutosha ambao wamejaa weledi wa kutoa huduma na wanaweza kuisaidia jamii.
Wizara ya Afya na TAMISEMI inapaswa kutoa ajira au nafasi kwa wanasaikolojia na wanasihi kuanza kutoa huduma kuanzia vituo vya afya hadi ngazi ya hospitali ya taifa ili kupunguza na kuzuia kuongezeka kwa wagonjwa wa Afya ya Akili au waathilika wa changamoto za kisaikolojia maana hawa watakua na watoa elimu na matibabu pia hasa matibabu ya awali ambayo hayahitaji dawa na kulazwa hospitali.
Wizara ya Afya, TAMISEMI na Wizara ya Elimu ziweke utaratibu wa wanafunzi kujua nadhalia kadhaa za juu ya Afy a Akili kwa kuanzia na shule za msingi, sekondari na vyuo kati na vikuu hasa kwa kuweka sheria zinazovitaka vyuo kuwa na watoa huduma za Afya ya Akili lakini pia wasimamizi wa wanafunzi (Deans) kuwa wanasaikolojia au wawe na mafunzo ya kutoa nasihi na sio ishauri tu kama wanavyofanya hadi sasa.
Wizara ya Afya katika maadhimisho ya kila mwaka ya Afya ya Akili Duniani itoe nafasi kwa wananchi kuhudhulia na wakutane na wataalamu na kujibu maswali waliyonayo vichwami mwao hapa maonesho ndiyo yanayotakiwa katika viwanja vya wazi na sio kwenye kumbi zinazoruhusu watu wenye miariko tu.
Hii pia itakuwa fulsa kwa taasisi zinazotoa huduma kufanya maonyesho na wadau wengine kujua zaidi kuwa huduma zipo nje pia ya hospitali.
Wizara ya Afya inapaswa kutekeleza sheria ya Afya ya Akili ya 2008 inayotaka bodi kufanya kazi na ni muda sasa kuwepo na bodi ya kusimamia watoa huduma wa Afya ya Akili na ihusishe Leseni na hii itasaidia kuondoa wadanganyifu katika kada ya Saikolojia na Afya ya Akili.
Mwisho niipongeze Wizara ya Afya kwa kuifanya Hospitali ya Afya ya Akili Taifa Mirembe kuwa taasisi inayotoa huduma mbalimbali za Afya ya Akili na mwili tofauti na hapo awali.

Upvote
3