Hali halisi ilivyo hivi sasa

BARAKA FESTUS

Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Niaje wakubwaa, Leo mwanajukwaa naweka mada mezani kuzungumzia sekta ya elimu,katika nyakati hizi kumekuwa na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia,lakini cha kusikitisha mfumo wetu wa utoaji elimu umeshindwa kuendana na kasi kubwa ya maendelo ya sayansi na teknolojia,ukiangalia shule zetu za awali na msingi zimekuwa na matatizo makubwa,na shule hizo ndio zinatakiwa zitoe elimu ya muhimu na ya msingi ambayo mtu anatakiwa awe nayo.

Kwa mfano embu jiulize mtu akimaliza shule ya msingi hajui kusoma,kuandika wala kuhesabu huyo mtu utampa kazi gani ataifanya maana hata mfyatua matofali anatakiwa kuhesabu ili ajue idadi ya matofali aliyoyafyatua,mwisho wa siku taifa litakuwa na watu wajinga hatimaye taifa haliwezi kuendelea. Miaka ya hivi karibuni,vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa wanaanza kidato cha kwanza lakini wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na hii inatokana serikali na jamii kwa ujumla kutolipa kipaumbele swala la elimu,kumekuwa na matatizo makubwa kwenye sekta ya elimu hasa elimu ya msingi na hasa matatizo makubwa yapo maeneo ya vijijini.

Moja ya tatizo ni, kutothaminiwa kwa fani ya ualimu kiukweli serikali haiwathamini walimu walimu wamekuwa wakiishi katika hali ngumu ya maisha kutokana na kupata mishahara midogo ukilinganisha na watumishi katika sekta nyingine mfano madaktari,mainjinia,wahasibu,kiukweli walimu wengi wanaofundisha shule za serikali hawawajibiki ipasavyo ukilinganisha na walimu wanaofundisha shule za watu binafsi,na hata ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na cha sita kumi bora zimetawala shule za watu binafsi. NI HAYO TU... Itaendelea............. From:TAJIRI WA FIKRA
 
hizo sera zako zinatosha kushawishi wapiga kura wakuchague mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…