Hali hii inanikuta mimi au watu wote?

Sio kwamba hutaki kuhamia bali kisaikolojia ubongo wako unapingana na mabadiliko.....uoga was kimabadiliko ni hali ya kimaumbile Kwa wanadamu......ndio maana.....waliofanikiwa zaidi kimaisha ni wale waliomua kwenda kinyume na utashi was nafsi zao kwani wakati mwingine nafsi hupotosha Kwa sababu ya uoga tu........

Ikarahishe nafsi na uhamie kwako baada ya muda utakuwa poa baada ya ku adapt mazingira mapya na kuyafurahikia......

Watu wengi hali hizi wanazihusianisha na uchawi hali ya kuwa si kweli hata kidogo......
 
Asante ..sana
 
Wanawake ndio wanapenda kulazimisha kuhamia nyumba uliyojenga

Yaelekea wewe huna mke
Mkuu yani hapa umeongea ukweli mtupu,mimi bila mke wangu nisingehamia kwangu Mivumoni kwa kweli,kwanza nilikuwa napaona mbali pili nilikuwa sijaweka tiles bado ila umeme nilikuwa tayari nimeshaweka,kuna siku wife akaniambia yani kodi hii ikiisha mimi nabeba vitu na watoto nitawakuta Mivumoni,kwa kweli mke wangu anamchango mkubwa sana wa kuhamia kwenye nyumba yetu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kabisa mkuu, mke ndo anahamasisha.
Mwanamke anakua na furaha sana kuhamia kwenye nyumba yake.
Ila kwa mimi nilie chelewa kuoa nikioa sasa hivi mke atasema tulichuma wote ikitokea labda tukaachana.
 
Hapana mkuu,nimejenga kahama vijijin. ila mim ni mkazi wa dar ndo nyumban ..kahama mambo ya utaftaji tu.

Hapo hakuna uchawi wala nini.


Ni kwamba tu wewe umejenga sehemu usiyoipenda, na inawezekana hata nyumba yenyewe umejenga ilimradi tu.. hujajenga nyumba ya ndoto zako. Ndio maana unaona uvivu kuhamia.

Kama vipi we ipangishe tu kodi utakayopata kule unalipa huku maisha yanaenda.
 
Nadhani ulinunua kiwanja eneo ambalo umepata kiwanja sio ulipo papenda, au usikute wakati ujenzi unaendelea ukagundua viashiria yakutokuwa sehemu nzuri kama majerani usio wapenda maana hata mimi nilinunua kiwanja sehemu ila nilipokuwa najenga nikaona kabisa kuwa siendani sawa na majiranj waliopo
 
Ukafanyaje boss [emoji846]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…