Hali hii mpaka lini?

Hali hii mpaka lini?

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
HPIM0462.jpg

Ni kawaida kuona wanasiasa wakiwarubuni wananchi kwa kuwapa maneno matamu sana na yenye matumaini hapo mbeleni. Lakini cha kushangaza utekelezaji wake ni karibia na kipindi cha uchaguzi ndo utaona hao jamaa wapo busy sana kuboresha vitu napo kwa kulipua.
Sasa hili Taifa la kesho linaweza kujengwa kati hali hii?
JK tembeza bakuri basi angalau Taifa la kesho lisikalie vitofauri na kukaa kwenye madarasa ya vumbi kama hili. Elimu ni jambo la msingi kwa binadamu kuliko bakuri unalo tembeza la vyandarua ambavyo vinaishia wa wajanja wachache na wewe ukiwa kimya.
Ukiwa kama mkuu wa kaya kuna changamoto kubwa mbele yako inua Elimu.
 
Komredi, inasikitisha kwa kweli. Ila hii hali JK kaikuta. Waliomtangulia wote nao waliikuta na hawakuweza kuibadilisha. Sasa hilo linaelezea jambo kubwa zaidi ya watu wengi wanavyodhania.

Bottomline ni kwamba, hii hali kwetu sisi haina mwisho. Leo miaka sijui 48 au 49 ya uhuru lakini hali hii bado ni rampant. Nakuhakikishia miaka 100 kuanzia leo hii hali itakuwepo tu.

Ndivyo Tulivyo. Mpende msipende.
 
Tuambie hii picha ya wapi na jimbo gani,ili tumtumie mbunge anayewakilisha jimbo hili,picha hii,na waziri wa elimu
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=it7cu5vyQ-g[/ame]

Mkuu anasema kuwa tumeweza kufuta ujinga.
 
hii ilikuwa enzi zile, hadi vibabu vijijini wanalazimishwa kusoma.
Kipindi hiko wizara ya elimu na watu wazima, kulikuwa na taasisi ya elimu na watu wazima...kina mama sitta walikuwa huko.
Wajanja walipoona nchi yoye inajua kusoma wakala hadi miradi...
Tanzania yangu, tunakoenda kubaya zaidi ya sasa....hatuna matumaini tena!
 
Tuambie hii picha ya wapi na jimbo gani,ili tumtumie mbunge anayewakilisha jimbo hili,picha hii,na waziri wa elimu

Hii ni reflection ya Tanzania nzima, isipokuwa miji yote katikati ya mji kuna afadhali kidogo, hiyo eception ni shauri ni wanataka iwe kioo cha nchi. Picha inatakiwa ipelekwe kwa wabunge wote inatia huruma kwa kweli. Tembeeni muone ndugu zangu.
 
HPIM0462.jpg

Ni kawaida kuona wanasiasa wakiwarubuni wananchi kwa kuwapa maneno matamu sana na yenye matumaini hapo mbeleni. Lakini cha kushangaza utekelezaji wake ni karibia na kipindi cha uchaguzi ndo utaona hao jamaa wapo busy sana kuboresha vitu napo kwa kulipua.
Sasa hili Taifa la kesho linaweza kujengwa kati hali hii?
JK tembeza bakuri basi angalau Taifa la kesho lisikalie vitofauri na kukaa kwenye madarasa ya vumbi kama hili. Elimu ni jambo la msingi kwa binadamu kuliko bakuri unalo tembeza la vyandarua ambavyo vinaishia wa wajanja wachache na wewe ukiwa kimya.
Ukiwa kama mkuu wa kaya kuna changamoto kubwa mbele yako inua Elimu.

hali hii itaendelea mpaka mimi na wewe au waTanzania kufuta ujinga wa kiakili na kutokuogopa. kama sio wewe ni jamaa yako ndio aliyeichagua CCM. kama sio mimi ni jamaa yangu ndio aliye ichagua CCM. Sasa tumlaumu nani CCM au sisi wenyewe. AİBU KAKA AİBU.
ENDELEENI KUİCHAGUA CCM halafu uje kulalamika hapa...
 
Hii hali itaisha labda mkoloni akija kutawala tena Tanzania.
 
Hii hali itaisha labda mkoloni akija kutawala tena Tanzania.
Kwani sasa hivi mkoloni hatawali? Hao watoto utasema wanajitawala? Mkoloni si lazima awe na ngozi nyeupe, lakini kikubwa zaidi si lazima akuambie 'Mimi ni mkoloni". Utaona mambo yalivyo tu, na utagundua kuwa unatawaliwa.
 
Back
Top Bottom