Tunaomba jamii ione na ipaze sauti kuhusu hiki Kituo cha Daladala cha Kigamboni, ona hali yake ilivyo.
Wilaya au wahusika wameshindwa kukijenga au? Kipo opposite ya Ikulu, kipo kwenye mlango wa bahari pahala ambapo ni Mjini kabisa, hali yake mbaya sana.
Tunateseka mvua zikinyesha, Mbunge yupo kimya, Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi kimya.
Ni aibu sana maana ndio kituo pekee ukitoka Mjini umevuka ndio kituo kilichopo. Kigamboni inatia aibu sana, viongozi hamna wanafanya kitu. Tusaidieni na watu waone jinsi walivyo. Tumewachoka hawa viongozi.
Tatizo la viongozi kupatikana bila ya ridhaa ya wapiga kura ndiyo hilo,wapiga kura wanakua hawana thamani kabisa,hata wakisemacho kinakua cha kijinga kabisa.Poleni sana wadau.