Hii inanikumbusha enzi zileee za treni ya kati. Tumesafiri na vizee vya kimang'ati tukafika ITIGI, kumbe kulikuwa na kibaka alimchomolea moja wao hela. Kidingi kikamshtukia wakati anashuka....wachaa weee! walianza kumpiga virungu vya kichwa....kibaka anatimua mbio kuelekea kituo cha polisi.....mpaka ndaniiiiii, wazee wanaendelea kumgonga tu na virungu, polisi wakazidiwa nguvu.....kibaka ndani ya meza lakini bado virungu vinamkuta!. Ndipo polisi walipowatishia bunduki hao wazee ndio wakaacha.....ilikuwa "live" burudani aiseee!