Hali inatisha Senegal kuliko watu nje wanavyojua

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka wanajamvi!

Kuna rafiki yangu msenegali ameenda kwao kumshughikia mke na mtoto wake Visa.

Tumewasiliana kwenye Whatsapp anavyonisimulia kwa kweli hali inatisha tofauti tunavyosoma kwenye vyombo vya habari.

Mjini Dakar mji mkuu wa Senegal hapaendeki. Mamia ya watu wameuwawa na vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini serikali inaficha Idadi.

Watu wameondoa hela zao benki hadi kuna uhaba.

Ofisi za umma mahospitali na balozi zote zimefungwa kupelekea huduma za jamii na za kibalozi kusimama na kudodora.

Senegal ilikuwa nchi, tulivu,
Stable na demokrasia.

Ni uroho wa madaraka wa viongozi wengi wa Kiafrika.

Mack Sally rais wa Senegal aliingia madarakani kwa kupigwa kura na vijana wengi na kuleta matumaini na demokrasia. Lakini akaja kubadilika.

Ni yeye alikuwa kimbelembele kumshurutisha na kumlazimisha jirani yake wa Gambia strong man Yahya Jammeh kuachia ngazi asikandamize demokrasia.

Chini ya wiki moja tu Senegal imebadilika na kuwa uwanja wa fujo.

Kuna uzi flani mwamba aliletaga humu kuhusu Senegal ulikuwa mzuri sana.

Tuwaombee ndugu zetu wa Senegal warudi kwenye utulivu na amani waliyoizoea.
 
Push back kutoka kwa middle class ambao wanajielewa na kuelewa on the ground kuko vipi, hapa unaweza Tia ndani KU na maisha yakaendelea!,ni mapigano ya walio nacho na wanaoona haki yao inaminywa,gharama za usawa ni jasho la damu
 
Ulafi ulafi na uroho na roho mbaya kwa viongozi na watu wengi weusi!

Na hata hivyo! Africa imelogwa! Ukipata viongozi strong, watawaita majina kibao, mara hitilla, mara dictater

Shauri yenu
 
Ulafi ulafi na uroho na roho mbaya kwa viongozi na watu wengi weusi!

Na hata hivyo! Africa imelogwa! Ukipata viongozi strong, watawaita majina kibao, mara hitilla, mara dictater

Shauri yenu
Yani mkuu unasema kweli. Huwezi kuamini leo hii wazimbabwe wamemmiss Robert Mugabe. Huwezi amini wa Gambia wamemmiss Yahya Jammeh.

Yani ndo maana naunga mkono tu PAKA atawale Rwanda hadi mauti.
 
Yani mkuu unasema kweli. Huwezi kuamini leo hii wazimbabwe wamemmiss Robert Mugabe. Huwezi amini wa Gambia wamemmiss Yahya Jammeh.

Yani ndo maana naunga mkono tu PAKA atawale Rwanda hadi mauti.
Ndio maana kila siku Tunaimba humu Demokrasia wabaki nayo huko huko Ulaya, tuna mifumo yetu ila Tunaikataa tunataka kuiga mambo yanayodidimiza tu Africa.

Ongezea na Gadafi hapo.
 
Senegal wazee wa tepolee tepoleee.... Hawa jamaa dakika mbili mbele wamekichafua na jirani zao Liberia.. Hii nchi Ina mkono wa mabepari sio bureee. Mana haipiti muongo bila rais kuharibu
 
Senegal na Tanzania tunatofautiana muda tu....

Hii miswada inayepelekwa kwa hati ua dharura ni roadmap kuelekea Dakar
 
Madaraka matamu
 
Ingawa hal
Ingawa hali ilikua tete last week ila kwa sasa hali imetengamaa kwa kiasi kikubwa.

Hali ya kutopatikana kwa hela ilitokana na mabank kufungwa na internet kuzimwa. ATM na mitandao ikawa haifanyi kazi.

Kwa sasa Dakar imerudi watu wanaenda makazini na bank zimefunguliwa.
Sijui miji mingine.
 
Dah mwaka Jana mwezi wa Saba nilikuwa Dakar Leo ..ni jiji Zuri sana ..siamimi kama Leo Ile amani niliyoiona pale haipo ..asee kumbe wale watu wakarimu ila watata ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…