DOKEZO Hali isiyoridhisha ya mazingira ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)

DOKEZO Hali isiyoridhisha ya mazingira ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
1: Barabara Mbovu na Mashimo Yasiyozibwa
Mara tu unapoingia kupitia geti kuu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pale mwanzo kabisa,(njia panda ya chuo) hali ya barabara sio nzuri sana . Barabara ina mashimo mengi, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa waendesha magari, pikipiki, na hata watembea kwa miguu.

Pia Eneo la junction ya utawala karibu na bank ya NBC, lina shimo ambalo limekuwepo kwa takribani mwaka mzima bila kufanyiwa matengenezo yoyote. Hili linaibua maswali kuhusu utendaji wa mamlaka husika na umuhimu wa kuweka vipaumbele katika uboreshaji wa miundombinu ya chuo.

Hali hii ni mbaya zaidi karibu na College of Education, ambako barabara imeharibika vibaya kiasi kwamba magari yanapata breakdown mara kwa mara. Ni jambo la kushangaza kuona kuwa ndani ya chuo kikuu, ambacho kinapaswa kuwa mfano wa maendeleo, kuna miundombinu mibovu kiasi hiki.
photo_2025-02-24_16-55-20.jpg

photo_2025-02-24_17-03-52.jpg
2: Ubovu wa taa za barabari inayopelekea kuwa Ukosefu wa Usalama Nyakati za Usiku
Katika maeneo kama vile karibu na geti kuu na barabara zinazoelekea katika sehemu za ndani za chuo, vibaka wamekuwa wakihatarisha usalama wa wanafunzi.

Hali hii inachangiwa na tatizo la taa za barabarani kutowaka, hivyo kufanya maeneo mengi kuwa yenye giza na hatari kwa watembea kwa miguu.

Taa za barabarani kutoka geti kuu hadi eneo la utawala ni mbovu, na hali hii inafanya hata wale wanaotembea kwa miguu kuhisi wasiwasi wanapokuwa njiani. Katika chuo kikuu kinachotegemewa kwa kuwa na usalama wa kutosha, hali hii haikubaliki na inapaswa kushughulikiwa mara moja.

3: Ukosefu wa Ukarabati wa baadhi ya Majengo ya chuo
Majengo mengi ya chuo, hasa yale ya zamani, yana hali mbaya kwa sababu ya ukosefu wa ukarabati. Baadhi ya majengo yana rangi zilizofifia au hata kupauka kabisa, na hayaonekani kuwa na hadhi inayostahili kwa taasisi ya elimu ya juu.

Swali linabaki: Kwanini majengo ya serikali, hasa yale ya taasisi kubwa kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hayawekwi katika hali nzuri?

Kutozingatia ukarabati wa majengo haya kunasababisha mazingira ya chuo kuonekana kuwa duni na yasiyo na mvuto kwa wanafunzi na wageni. Katika nchi nyingi zilizoendelea, vyuo vikuu huwekeza sana katika kuboresha mandhari na miundombinu yao, lakini hapa kwetu, hali inaonekana kudorora bila hatua za haraka kuchukuliwa.

Hali isiyoridhisha ya mazingira katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni suala linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Barabara mbovu, ubovu baadhi ya taa kwa usalama na ukosefu wa ukarabati wa majengo ni changamoto ambazo haziwezi kupuuzwa.

Mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa chuo hiki kinakidhi viwango vya taasisi ya elimu ya juu.
 
Back
Top Bottom