Hali mbaya Clouds media,wakubali yaishe kwa WCB..

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Katika kile kinachoonyesha maji yamewafika shingoni Clouds media wametoa kauli nzito kupitia kwenye page ya Shilawadu(hapa nadhani wameamua kuficha aibu kwa kupost bandiko kwenye akaunti ya shilawadu badala ya akaunti official za cloudsfm au tv).
wanadai ni vyema media\matamasha yasimame yenyewe bila kutengeneza uhasama na wao kwani kila.mmoja anaweza kufanya mambo yake na akapata pesa bila kutengenezeana chuki.

Swali:Je nani kati ya Clouds na media nyingine au wasanii nani ni kinara wa kutengeneza migogoro?
 
Zaidi ya wanamuziki 30 wanatarajiwa kushiriki katika tamasha la fiesta linalotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kamati ya Maandalizi, Gardner G Habash, alipokuwa akizungumzia tamasha hilo.

Habash amesema mpaka kufika leo wasanii 30 tayari wamesajiliwa na wengine bado wataendelea kuwasajili hadi siku ya Jumamosi asubuhi.

Akielezea mafanikio ya tamasha hilo tangu lianze amesema anashukuru limekuwa la mafanikio ikiwemo kupokelewa vizuri katika kila mahali walipopita.

Pia, wasanii amesema wamekuwa wabunifu tofauti na huko nyuma na pia wamekuwa wakiishi kwa kushirikiana na kupendana.

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo wadhamini wakuu wa tamasha hilo, William Kapinga amesema kiingilio katika tamasha hilo ni Sh15,000 kwa watakaolipia getini na Sh10,000 kwa watakaolipa kwa tigopesa.

Wakati wale watakaotumia usafiri wa Uber kwenda katika tamasha hilo na wakati huohuo wakiwa wamelipa kwa tigopesa watapata punguzo la Sh5000.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii, Joh Makini, amesema wakazi wa Dar es Salaam wategemee mambo makubwa katika shoo hiyo kwani kila walipopita wameacha alama hivyo hata katika Jiji hilo watarajie mambo mazuri pia.
 
Ushindani muhimu sisi watazamaji na wasikilazaji
 
Clouds hawana uswahili. Wapo kimya mtaona tu mambo yanavyonyooka. Ruge is genius hasemi,hajibu wala koment. Kimya kimya matokeo ndy hujbu
 
Clouds hawana uswahili. Wapo kimya mtaona tu mambo yanavyonyooka. Ruge is genius hasemi,hajibu wala koment. Kimya kimya matokeo ndy hujbu
Umesahau #mkubwakasema kipindi kile Ruge alivyopiga marufuku nyimbo za Jide, Umesahau Jide anazindua album yake nao siku ya tarehe hiyo wakapanga event ya mwana FA ili wazuie wasanii wasiende kwenye uzinduzi wa Jide, Umesahau CMG walichomfanyia Majizo kupanga tarehe moja, mkoa mmoja siku ya pili Gerrard Hando, Kibonde na Adam mchomvu wakawa wanamponda kimafumbo Majizo, CMG ni waswahili tena waswahili haswa na fitina wanazijua, sema sasa hivi wamekutana na mswahili mwenzao na ndio maana waswahili wanasema usipende kuwafanyia wenzio kile usichokipenda kufanyiwa ww.
 
Wakati ukuta... Wakati si milele... Hata umri una kikomo... Umri sio miaka. !
 
Walikuja Efm hivi-hivi na kelele nyingi baadaye wakapotea.

Clouds Madia ni Giant na siku zote Giant hawezi kudondoshwa kwa makelele ya Konyagi za Konki Master.
 
Kila media inayokuja inataka kujipima ubavu na clouds, clouds wamezoea kuupisha upepo baada ya muda ndio tunajua clouds still ni giants wa burudani hapa bongo, kuishusha clouds sio kelele hizi za mtandaoni bali ni kuandaa content zilizoshiba ili kuipoteza “power breakfast, leo tena, XXL, Jahazi, Amplifaya, Sports Extra na Hara za roho. Yaani media ambayo ukiambiwa umtaje presenter mkubwa unajibiwa jonijo ndio ushindanishe na clouds😳😳?

Wasafi wanahitaji miaka zaidi ya mitano ili kuandaa content ya kufanya watu wasifungulie 88.5 asubuhi kusikiza power breakfast.

Nb; Hivi mnashindanisha vipi show innayopigwa mtwara na inayopigwa dar? Mi naona hizi ni stratergies za ku gain popurality na wefanikiwa kwa asilimia zote
 
Mjomba huu mchezo usiuchezee kabisaaaaaaa
 
Miaka mitano, yakwako tusubiri miaka mingapi ???
 
Nondo hizo safi sana.. facts hadi unasema pooooo.. kweli amewashauri vizuri sana.. kama hawajaelewa basi watajiju
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…