KERO Hali mbaya ya barabara ya Nyanguge - Ndabaka Gate (Bunda) inasababisha adha kwa wasafiri, Safari ya saa 1 inachukua saa 4

KERO Hali mbaya ya barabara ya Nyanguge - Ndabaka Gate (Bunda) inasababisha adha kwa wasafiri, Safari ya saa 1 inachukua saa 4

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Wasafiri mnaopitia barabara hii hakika wanaona adha kubwa na taabu na uharibifu mkubwa wa barabara hii. Barabara hii ilijengwa na kuisha mwaka 1980 na Kampuni ya Lanari ya Italia na tangu wakati huo hakuna marekebisho aina yoyote yaliyofanyika..

Kwa mwendo wa kawaida kutoka Nyanguge mpaka Ndabaka Gate (Bunda) ni mwendo wa saa moja lakini kwa hali ilivyo sasa inakuchukua masaa manne. Kanda ya Ziwa ina Wabunge kwenye Bunge letu na wanapita kwenye barabara hii na hakuna wanachofanya.

Barabara hii imechukua miaka mingi bila kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote.

Ninaiomba Serikali itenge bajeti kubwa na kipande cha barabara hii kifumuliwe chote na kujengwa upya kabisa.

Kwa kweli ni adha kubwa kwa wasafiri wanaotumia kipande cha barabara hii.
 
Kwa makamu wenyeviti huko,yaani Heche na rafiki yake Wasira,bilashaka watalimaliza hilo tatizo.
 
Hyo barabara ndo highway mbovu inayounganisha mikoa kuliko highway zote Tanzania
 
Back
Top Bottom