Hali ngumu ya uchumi imenifanya nitafakari tulikotoka na tunakokwenda

Hali ngumu ya uchumi imenifanya nitafakari tulikotoka na tunakokwenda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ile miaka yetu wahenga mama zetu wengi walikuwa wake na mama wa nyumbani. Wengi walifika kuanzia darasa la nane na kuendelea. Enzi za elimu ya mkoloni cookery na needle work yalikuwa masomo compulsory kwa mtoto wa kike.

Mishahara ya wazazi haikuwa mikubwa sana lakini wengi tulibahatika kuishi kwenye government quarters zenye umeme na maji. Mama alifuga kuku kidogo na alipanda mchicha.

Mama wengi walikuwa na vyerehani ndani ya nyumba. Shule zikikaribia kufunguliwa mama anakwenda kununua vitambaa Kisutu au Kariakoo na mnashonewa sare za shule. Mama alishona mapazia na shuka pia. Haya aliyafanya katika muda wake wa kupumzika hasa mchana.

Wakati wa birthday mama alioka keki, hata kama hakuna party kubwa lakini jioni inawekwa keki na orange juice na mwenye birthday anaimbiwa. Unajisikia vizuri.

Elimu ya sasa haimuandai mtoto katika ubunifu wa kuokoa pesa. Maisha yamekuwa magumu kwakuwa tunayaongezea ugumu.
 
Back
Top Bottom