WanaJF,
Kwa siku ya nne (4) hostel za Mabibo hazijafanyiwa usafi na watoa huduma wa kampuni mojawapo iliyoingia mkataba na chuo kikuu cha Dar es Salaam kufanya hivyo.Taarifa zilizozagaa ni kwamba wafanyakazi hao (vibarua) wapo kwenye mgomo dhidi ya mwajiri wao wakiwa na madai mbalimbali mojawapo likiwa la kutokulipwa mshahara wao wa Januari hadi sasa. Sasa kutokana na hali hiyo hali ya corridor na vyoo ni mbaya sana. Kuanzia jana wanachuo walianza kujimobilize na kutaka waonane na uongozi wa chuo juu ya mstakabali wa afya zao.