Habari za jioni ndugu zangu wapendwa wa mtandao huu wa JF kupitia Jukwaa hili mahsusi la Jamii Health. Naamini tuko hapa kwa ajili ya kuelimishana na kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali kwenye vichwa vyetu - Yote ni katika kukabiliana na changamoto za kila siku za kimaisha. basi bila kupoteza muda ningependa kwenda moja kwa moja kwenye kile kilichonileta hapa nikihitaji ushauri mzuri kutoka kwenU utakaoweza kuleta matokeo chanya.
Kwa ufupi ni kwamba, mama yangu mzazi anasumbuliwa na tatizo la kiafya ambalo kitaalamu linafahamika kama SYNOVIAL FLUID au KUPUNGUKIWA NA UTE KWENYE MAUNGIO YA MAGOTI. Hadi Sasa ameshafanya vipimo vingi ikiwemo cha MRI Scan ambacho kilimtaka afanyiwe operesheni ya miguu yote miwili, hali iliyopelekea kumnyima raha hasa ukizingatia yupo above 50+. Sasa kuna mzee m1 jirani yetu alitoa ushuhuda kwamba aliwahi kuumwa na kufikia hatua kama yake.
Akasema kwamba kuna shirika moja hapa mjini linaitwa WEST INTERNATIONAL walimuagizia virutubisho kutoka Ujerumani vinavyoitwa EDGE ambavyo vilimgharimu takribu Tzs 1.2M za kitanzania hadi kumfikia na hadi sasa anaendelea vizuri. Kitu kilichonipa wasiwasi ni kwamba nilipojaribu kumuambia anielekeze ofisi zao alidai kwamba ni muda mrefu umepita wamehama na hana mawasiliano yao ila kama tunahitaji anaweza akafanya namna akatuletea kwani kuna package moja imepaki. Binafsi sikulihafiki hilo ndio kupelekea hadi kuja hapa kuomba ushauri kutoka kwenu.
kwa yeyote anayefahamu dawa, tiba, au virutubisho vitakavyoweza kusaidia kupona hili tatizo basi asisite kunishauri - kwani waswahili wanakwambia ugonjwa usikie kwa mwenzako na ombea usikufike. Nina imani kubwa ya kupata ufumbuzi kupitia jukwaa hili kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Niwatakie Jioni Njema Wote.
NAWASILISHA