KERO Hali ya barabara jimbo la Kibamba mkoani Dar es Salaam ni mbaya sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Wakati mwingine watu wanajiuliza hili jimbo lilianzishwa kimakosa? Barabara zote muhimu ni chakavu na sio za lami.

Nilipita barabara ya kibanda cha mkaa kwenda mjimpya nikajiuliza hili jimbo lina Tarura? Na kama Tarura ni wazembe mbunge na diwani na hata chama tawala wako wapi?

Kimsingi hili jimbo lipo kwenye auto pilot na CCM italipoteza kwa hali iliyopo sasa.

Hakuna mbunge wala diwani.
 
ninyi wananchi muishio kibamba hamna tofauti kubwa na sisi wa jimbo la segerea ni kama tumekosa muwakilishi.
 
Kwa kweli hata mimi siku ya kwanza kufika hilo jimbo nilijiuliza sana maswali mengi! Jimbo hilo halipaswi kuwa ndani ya Mkoa wa Dar.
 
well noted,
Poleni sana
 
Ukimuona Jery Slaa anavyojifaragua kwenye tv utafikiri amefanya cha maana sana hapa Ukonga
 
Mpiji magoe ndo kufika ni kisanga, soon tutakimbia vibanda vyetu....
 
Kizimkazi hana muda na watanganyika
 
Ukienda Msumi na Mpigi magohe nd'o utalia.
 
Huku CHADEMA wakishindwa kubeba jimbo...nitajua ni ule utchawi wa kimakonde. 👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…