KERO Hali ya barabara kuu Njombe - Songea kuanzia eneo la Soko Kuu hadi Uwanja wa ndege ni mbovu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

waterproof

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2020
Posts
388
Reaction score
352
Hali ya barabara kuu ya Njombe–Songea, kuanzia eneo la Soko Kuu la Njombe hadi Uwanja wa Ndege wa Njombe Mjini, imezua malalamiko kwa wakazi na watumiaji wa njia hiyo baada ya kuharibika na kugeuka tope kufuatia matengenezo ya viraka.

Inadaiwa kuwa matengenezo yanayofanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Njombe yamehusisha matumizi ya tope kuziba mashimo, jambo lililosababisha barabara hiyo kuwa na hali mbaya hususan kipindi cha mvua. Hali hiyo imekuwa ikihatarisha usalama wa watumiaji wa barabara, wakiwemo madereva wa magari,watembea kwa miguu na waendesha pikipiki, pamoja na kuongeza usumbufu wa usafiri katika eneo hilo.

Baadhi ya Watumiaji Wa Barabara hiyo wameeleza wasiwasi wao wakidai kuwa njia hiyo ni muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo wanaiomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kufanya matengenezo ya kudumu badala ya viraka visivyodumu

 

Attachments

  • PXL_20260228_095151200.jpg
    983.5 KB · Views: 37
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…