A
Anonymous
Guest
JF tunaomba mtusaidie kupaza sauti kwa Serikali ya Kigamboni kuhusu changamoto ya barabara, kwa kweli ni mbovu sana hasa maeneo ya Kwa Fundi Baiskeli.
Mvua zikinyesha baada ya hapo hayo mashimo waliyoyafunika yanarejea kama awali na wakati mwingine yanaweza kuwa makubwa zaidi.
Kinachokera zaidi wameweka bango la Mkandarasi kuwa wanatengeneza Barabara tangu Aprili 2024 ila mpaka kufika leo hii, hiyo barabara inazidi kukatika na hakuna kinachoendelea.
Soma Pia: Mkandarasi wa barabara ya Majichumvi-Migombani anatutesa kwa zaidi ya Mwezi sasa
Watumiaji wote ikiwemo Bodaboda na watembea kwa miguu wote tunateseka kwa kiasi kikubwa sana. Serikali iangalie kinachoendelea huku, kama hilo bango la Mkandarasi limeweka kama pambo waje walitoe tu.