DOKEZO Hali ya Choo cha MV KOME II ni hatari kwa afya na usalama wa Watumiaji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kivuko cha MV KOME II kinachofanya safari zake kati ya Nyakarilo na Kome Kisiwani katika Halmashauri ya Buchosa, Wilayani Sengerema naweza kusema kinawafanyia ukatili abiria wanao tumia usafiri huo.

Kivuko hicho kwa sasa hakina huduma bora ya choo kwani choo kilichopo ni kibovu kimejaa matobo, ukiingia ndani kujisaidia huwezi kujitofautisha na mtu anayejisaidia hadharani kweupe.

Choo kilichopo ndani ya kivuko hicho hakifai kwa matumizi ya binadamu mwenye akili timamu, mbali na matobo lakini kinatoa harufu kali jambo ambalo ni kero kwa abiria ambao wataketi karibu na choo hicho na mbaya zaidi kama mtu ataingia kujisaidia haja kubwa basi harufu yote ya ndani itahamia nje.

Kupitia jukwaa hili naomba TEMESA na viongozi wa Serikali tuwafikishie ujumbe huu ili hatua za haraka zichukuliwe ili kunusuru vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa abiria wanaotumia kivuko hicho.

Tupingeni kwa nguvu zote vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika kivuko cha MV KOME II kwani ni ukatili kama ukatili mwingine.

Kingine, milango ya feli inayotumiwa na abiria pamoja na magari imekatika na mara nyingi inategemea cheni sasa hofu ya sisi watumiaji ni endapo siku ikikatika hiyo minyororo mambo yatakuwaje?

Pia, chumba ambacho huhifadhi life jacket (vifaa vya uokozi) mara nyingi huwa yanapaki magari pale na kuziba mlango sasa watumiaji tunajiuliza je siku ikitokea kivuko kikapata changamoto abiria wanaweza kujiokoa kwa namna ipi?

Kivuko cha MV KOME II hufanya safari zake kwa upande wa KOME mara tano na upande wa Nyakarilo mara tano kwa siku, hivyo takribani hufanya safari mara 10 kwa siku na kimekuwa kikilalamikiwa kwamba kimekuwa kikibeba abiria na magari zaidi ya uwezo wake na ndiyo maana kuna wakati hupigwa na mawimbi na kupoteza njia.
 
Usichukulie poa, nyumba ni Choo kumbe haifanyi Kazi kwenye vivuko.
Ila Watanzania kwenye maintenance tupo nyuma sana, Yani hata marekebisho ya choo.
Unaweza panda Ndege zetu ukakuta chooni hata maji hakuna. Kama vyoo vya treni.
 
Ni kawaida ya Serikali za Kiafrika kuniglect kufanya Maintenance kwenye vyombo vyake hata Vyoo vya SGR vitaishia kuwa kama hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…