Hali ya Elimu katika Nchi Yetu Sasa

Hali ya Elimu katika Nchi Yetu Sasa

Joined
Apr 5, 2024
Posts
81
Reaction score
117
children-smiling.jpg

Habari wanajamvi,

Naamini tunaendelea vizuri na shughuli zetu za kufunga mwaka wa 2024. Mungu amekuwa mwema kwetu, na ni kwa kudra zake tunaendelea kuishi.

Jana nilimtembelea rafiki yangu mmoja. Yeye na mke wake ni waalimu wa sekondari. Tuliongea mengi, na mojawapo ya tulivyovigusia ni hali ya elimu nchini kwa sasa.

Mwalimu, anayefundisha mjini alituambia kuwa wanapata changamoto moja mpya siku hizi. Anasema kuwa baadhi ya watoto wa form 1 hawawezi kuandika majina yao vizuri.

Nilivyofundishwa, jina langu hutangulizwa na herufi kubwa. Samedi Amba. Sasa, naambiwa kuna watoto wa form 1 ambao wangeandika jina hilo hivi "samEDI AmBA". Yaani, anachanganya herufi. Hajui tofauti kati ya herufi kubwa na herufi ndogo.

Hali katika shule ya Msingi
Mke wa mwalimu akachangia mada. Yeye anafundisha shule ya sekondari ya kata. Akatuambia kuwa mapema mwaka huu, alikuwa msimamizi katika mitihani ya shule ya msingi ya darasa la 4.

Akagundua kuna watoto wa darasa la 4 hawajui kuandika majina yao. Yuko darasa la 4. Hawezi kuandika jina lake. Wasimamizi wanalazimika kuwajazia majina yao kutumia orodha ya majina ya mtihani.

Nilishtuka sana. Nkakumbuka jinsi mimi na mke wangu tulikuwa tukijadili kama tunaweza kuwapeleka watoto shule za serikali (tunao watatu) ili kusoma halafu tukawapa tuition ya Kiingereza.

Naambiwa kuwa mitihani ya sasa sio shading tena (yaani chagua mojawapo). Wanalazimika kuchakata na kuandika jibu (process based exams). Naambiwa kuwa mwaka huu watahiniwa wengi sana wamefeli kwa badiliko hili tu.

Shule za Private...
Tugeukie upande wa pili. Shule za private, AKA mabasi ya njano.

Ni tamanio la kila mzazi kumpa mtoto wake elimu nzuri. Hasa kwa mujibu wa lugha ya kiingereza, ambayo ishaonekana kuwa janga la taifa.

Shule hizi, ambazo pia zinaitwa ENGLISH MEDIUM, zimeonekana kujizatiti kuwasaidia wanafunzi kupata wanachokikosa katika shule za serikali.

Ila, ikumbukwe kuwa changamoto zipo kila mahali. Kwanza, imeonekana kuwa system hizi mbili zinagongana (not compatible).

Kwa mfano, kuna shule ya chekechea hapa jirani ambapo jamaa yangu mmoja alipeleka mtoto wake. Alikuwa na malengo ya kumpeleka shule ya private.

Lakini kwa kuwa maisha hayatabiriki, akabadili nia angani. Alipompeleka shule ya serikali, mwalimu akapata shida. Mzazi akaambiwa kuwa mtoto "alikuwa mjuaji". Kiingereza anaupiga mwingi. Anamrekebisha mwalimu katika kila kitu. Ikabidi apewe tuition kwa ajili ya kuendana na mfumo, na "kupunguzia makali".

Pili, mitihani.

Kuna mwalimu alikiri kuwa kuna baadhi ya shule wanaibiwa/kufundishwa mitihani. Au niseme kuwa wananunua mitihani. Mtoto anaonekana kuwa amepasua. A kama zote. Shangwe nyumbani. Lakini bado vipimo vya ziada vikifanywa, anaonekana kupungukiwa vitu fulani.

Kuna shule za chekechea mwalimu humjazia mtoto majibu ili mzazi asiyefuatilia aamini kuwa mtoto wake anaelewa.

Mzazi mwingine akaambiwa kuwa ili mtoto aweze vizuri, alipie tuition ya ziada.

Tuition
Nikadhani suluhisho ni tuition. Kila nkitoka kazini, nakutana na wanafunzi wa shule za private wamepangana kusoma "evening classes" yaani tuition. Jirani yangu ni mwalimu, na anakiri kukusanya "mia mbili, mia mbili" kwa wanafunzi wanaobaki jioni kusoma twisheni.

Nkajiuliza kuwa hawachoki hawa? Siku nzima mtiti, jioni darasa. Wanalala saa ngapi? Hawasaidii kazi za nyumbani hawa?

Hapa Kazi Tu
Ni mwezi wa 12 sasa, likizo ya krismasi ambapo wanafunzi wanahitajika kupumzika na kujipanga kwa mwaka mwingine wa masomo.

Ila? Twisheni. Kuna shule moja jirani hapa, darasa la 3 (wanaosubiri kwenda la 4 mwakani) wanasoma tuition. Darasa la 5 (ambao wanapaswa kuingia la 6 mwakani) wanasoma tuition.

Pamoja na tuition zote hizo bado tuna pre-from 1, pre-form 3 na pre-form 5. (Nasikia zimekuwa za lazima). Sahivi wajasiriamali wa elimu wanapiga hela na pre form hizi.
Tena tusipoangalia tutakuwa na pre-university (huenda ipo tayari).

Kwa nilichokisikia, sio salama. Lakini, tuwe wazalendo pia. Huyo mtoto asiyejua Kusoma, Kuhesabu na Kuandika, atakuwa mtumishi siku moja. Na atahudumia katika mambo fulani katika jamii. Nani ajuaye, anaweza kuoa binti yangu mojawapo.

Huyo asiyemudu KKK, atapewa uongozi, aidha wa serikali au katika sehemu yoyote ile. Of course huduma hutegemea uelewa kuliko usomi, lakini kuna vitu vya kuvifahamu pia. Je, atakuwa exposed vya kutosha, kwa kusoma na kuelewa, na kuongoza vyema?

Na wa mabasi ya njano ajuaye kusema kuliko kusoma na kuandika, pia yupo hatarini (shida ya wakenya hii itatukuta pia. Hata hivyo, tunawakubali sana walimu wao kuwafundisha watoto wetu).

Nikaendelea kujiuliza maswali kadhaa.

Kwa shule za serikali
1. Kwani, watoto huwa wanajifunza nini shuleni.
2. Walimu wetu katika shule za serikali, wanatumia mbinu zipi kufundisha. Hasa wanapolazimika kutumikia halaiki kubwa ya wanafunzi.
3. Wazazi je? Tunafanya sehemu yetu? Au ndo tukiwapeleka shuleni tushamaliza?

Kwa shule za binafsi
1. Nini zitafanya shule hizi kuendelea kuvutia, tofauti na Kiingereza?
2. Nini kifanyike kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa vizuri, na wazazi hawadanganywi na marks ambazo sio halisi kwa baadhi ya wanafunzi?

Kwa ujumla
1. Je, tutawin kwa kuwa na tuition nyingi iwezekanavyo?
2. Nini kifanyike kuipa elimu ya Tanzania mvuto, nguvu, na relevance (muktadha) katika dunia ya leo inayoenda kwa kasi ya sayansi, teknolojia na akili mnemba?
3. Vipi kuhusu skills (uwezo na ujuzi halisi). Lini tutawafundisha on-demand skills za biashara, kazi za mikono na teknolojia.

Hebu tuongee. Maoni yako ni yapi?
 
Achia mbali hizo KKK na jinsi ya kuandika majina yao, kuna mwamba wa kidato cha kwanza nilimuuliza umri wake akasema hajui maana mama yake hajamwambia.

Na miamba kibao ya kidato cha pili ukiiambia ihesabu 1 hadi 50 tu kwa kiingereza haitoboi

Lakini karibu kila mwaka takwimu za NECTA zinaonesha ufaulu umeongezeka.

Siasa zishaingilia mambo ya elimu, sisi hata tuseme vipi hakuna litakalofanyika kama halina manufaa kwa wanasiasa uchwara.
 
Back
Top Bottom