Hali ya joto kali bara la Ulaya (Europe)

Hali ya joto kali bara la Ulaya (Europe)

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2019
Posts
15,954
Reaction score
35,415
Wakuu hili joto kipindi hiki ulaya ni kwanini inatokea hivyo, huku kwetu ni baridi na maeneo mengine ni baridi kali kwelikweli, Mbeya, Arusha, Moshi, Kagera, Iringa(baadhi ya maeneo), Njombe(Makete), hali ni tete. Baridi maeneo hayo ni kali mno.

Hadi baadhi ya wananchi wa maeneo ya jiji la biashara Dar es salaam wanalalamika juu ya baridi huko.

Lakini huko Ulaya ni joto mpaka wanataka kukimbia, wajuzi wa mambo naomba mtujuze kwanini hali hii inatokea??
Kuna ihusiano wowote na nort/south pole ya hii dunia (duara).?

Na wenye updates za zile nchi zenye baridi kali kama Canada, Finland, Iceland etc, watupe tujue huko nako kunakuaga na kipindi cha joto kali kama mwezi wa 8, 9 au 10 nchini kwetu au miezi hii huko Ulaya.

Soma hii habari pia...
Maelfu ya wataalamu wa zima moto wanaendelea kukabiliana na janga la moto katika nchi za Ureno, Hispania na Ufaransa, huku wimbi la joto kali likionyesha kutokuwa na dalili ya kupunguza.

Kaskazini mwa Ureno, rubani alifariki wakati ndege yake ya kusaidia shughuli za zima moto ilipoanguka katika eneo la Foz Coa, karibu na mpaka wa Hispania. Mamlaka ya Ureno inasema takriban watu 238 wamekufa kutokana na joto hilo katika wiki iliyopita.

Moto unateketeza maeneo ya kusini-magharibi mwa mkoa wa Gironde nchini Ufaransa, ambapo zaidi ya watu 12,000 wamehamishwa.

Vipindi vya joto vimekuwa vikitokea mara kwa mara, kukileta wimbi kali zaidi la joto, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za binadamu.

Kwa sasa joto duniani limeongezeka kwa takriban nyuzi joto 1.1C tangu enzi ya viwanda ianze na halijoto itaendelea kuongezeka kama serikali kote ulimwenguni hazitafanya juhudi za kupunguza kiwango cha uzalishaji wa kaboni.

Mamlaka ya hali ya hewa Ufaransa imetabiri viwango vya joto vya hadi nyuzi joto 41 katika sehemu za kusini mwa nchi siku ya leo Jumapili na rekodi mpya za joto zinatabiriwa kuendelea kesho Jumatatu.

Mkazi mmoja kusini-magharibi mwa Ufaransa alielezea moto mkubwa uliozuka msituni kama hisia "baada ya apocalyptic" - "Sijawahi kuona hii hapo awali," Karyn, anayeishi karibu na Teste-de-Buch, aliliambia shirika la habari la AFP.

Waziri wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin alisema moto hadi sasa umeteketeza hekta 10,000 (ekari 25,000) za ardhi na kusifu "ujasiri wa ajabu" wa wazima moto.
Credit to @Bongo5Updates



FB_IMG_1658064785791.jpg

NB. Naomba tufundishane naamini hakuna anaejua kila kitu hii dunia. Tusidharauliane kwa kutojua kwetu.
 
Kwanza dunia hauko kama tufe bali iko kama yai kutoka Katikati ya dunia kwenda kas ama kus ni mbali kuliko kutoka kati mpaka magh ama mash

Dunia imekaa tenge kwa nyuz 33. Simu yangu imepasuka kio inasumbua
 
Limefikia nyuzijoto 40 hali NI mbaya Spain joto limesababisha mtambo upate shoti Moto ukatokea Sasa hivi unaunguza msitu watu takriban 14000 wamehamishwa.

Pia UK, Ufaransa na Ureno hali ni mbaya
 
Mnakumbuka tulianza na covid, tukaja na uhaba was mafuta na gas monkeypox kisha gharama za maisha kupanda? Tukaja na kitisho cha nyukilia na WW3 sasa tupo na joto, mpaka mbaki 1bn Alisikika mtu mkubwa akisema huko ulaya.
 
Kwanza dunia hauko kama tufe bali iko kama yai kutoka Katikati ya dunia kwenda kas ama kus ni mbali kuliko kutoka kati mpaka magh ama mash

Dunia imekaa tenge kwa nyuz 33. Simu yangu imepasuka kio inasumbua
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom