Hali ya kusikitisha: Majitaka yajaa na kutiririka kila mahali katikati ya Jiji la Nairobi

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Your browser is not able to display this video.

Hali ya usafi katikati ya Jiji la Nairobi inazidi kuwa mbaya kutokana na maji taka kutiririka hovyo mitaani. Miundombinu mibovu na mifereji iliyoziba imesababisha maji machafu kujaa barabarani na kwenye maeneo ya wazi.

Hali hii inawasumbua waenda kwa miguu, wafanyabiashara na wakazi wanaopita eneo hilo kila siku, huku harufu kali na uchafu vikihatarisha afya za wananchi na kuchafua mazingira.

Je, mamlaka zinazohusika zinasubiri nini kabla ya kuchukua hatua kurekebisha mifumo ya maji taka na kuzuia hali hii isiendelee kuwa tishio kwa afya ya umma?

Una maoni gani kuhusu hali ya usafi na miundombinu katikati ya Jiji la Nairobi?
 
Nchi za afrika mashariki zinafanana kwa uchafu.kariakoo Tanzania kila siku chemba za majitaka zinavuja na hakuna hatua inayochukuliwa miaka na miaka
 
Hili ni eneo gani? Location?
 
duh, hapo sijui nani kamzidi mwenzake kwa maana dar mvua zikinyeshwa ndiyo wanafungulia vyoo hivyo maji ya mvua yanayotiririka yamechanganyika na maji taka ya choo vs nairobi bila ya mvua maji taka yanatiririka mitaani hapo ni pepsi vs coca ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…