Network Engineer 2
New Member
- Sep 1, 2022
- 2
- 10
Naitwa Network Engineer, mzaliwa wa Wilaya ya Iringa. Nilizaliwa mwezi Agosti mwaka 1989 mama yangu akiwa nyumbani kwa bibi kwakuwa walikuwa hawajaoana na baba. Malezi yangu na mama yangu yalikuwa mikononi mwa bibi yangu. Nilipokua kidogo mama alibahatika kuolewa na baba mwingine (baba mlezi) ambaye katika harakati za kutafuta maisha mwaka 1995 waliondoka Iringa na kuhamia mkoani Mbeya nikabaki na bibi. Baba yangu mzazi alikuwa kijiji kilekile lakini alikuwa na familia yake na mambo yake!
Kutokana na changamoto kipindi kile, mawasiliano na wazazi wangu hayakuwepo kabisa, tulikuwa tunasikia kuwa wapo eneo linaitwa Makongolosi. Mwaka 1998 nilianza shule ya msingi nikiwa mikononi mwa bibi yangu kipenzi. Alinisisitiza nijue kusoma na kuandika tupange safari ya kwenda huko Mbeya kumtafuta mama. Kwakuwa bibi alikuwa hafahamu kusoma hivyo mimi nitasoma majina ya vibao na maeneo tukiwa njiani na hatutapotea.
Kutokana na uwezo mdogo wa bibi alijikita zaidi kunitafutia chakula na mahitaji ya shule,nakumbuka kipindi kile tulikuwa tunalipa ada shule ya msingi ambayo ilifutwa mwaka 2000 kama sijakosea nikiwa darasa la tatu. Kwa miaka yote sijawahi kulipa ada pamoja na kucharazwa viboko mara kwa mara na kurudishwa nyumbani kufuata ada. Nikiwa darasa la pili bibi alilazimika kwenda kutafuta shamba kijiji cha pili ili tuweze kulima. Nilibaki nyumbani peke yangu,alirudi mara kwa mara kuangalia usalama wangu na kuniletea unga na mboga. Wakati natoka shule nilikuwa napitia kwenye shamba la mwalimu wa Kiswahili ambaye alikuwa anavuna karanga hivyo nilikuwa nafanya kazi nayeye ananinunulia daftari ili kumpunguzia mzigo bibi.
Nilipofika darasa la tano mwaka 2002 mama na familia yake walirudi Iringa. Ni kama ulikuwa muujiza maana haikutegemewa na walikuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yetu. Lakini katika hali isiyoeleweka tulianza kuugua mara kwa mara na hali ya uchumi ikadidimia tena, baba yangu mlezi aliendelea kumsaidi bibi kuhakikisha japo napata mahitaji ya shule pamoja na wadogo zangu wa mama mmoja.
Mwaka 2003 mwishoni nikiwa darasa la sita baba mlezi alianza kazi ya kwenda kununua samaki Mtera na kuuza kijijini akiwa na mwenzake mmoja. Walikamatwa na askari wa maliasili kwa madai kibali kilikuwa kimekwisha muda wake. Walifunguliwa mashitaka mahakamani Iringa mjini. Baada ya wiki moja waliachiwa na kuamriwa kuripoti kila mwezi mahakamani wakati upelelezi unaendelea huku wakiacha baiskeli huko. Hali ya maisha ilizidi kuwa mbaya kwakuwa jukumu jipya liliingia kutafuta nauli ya basi kwenda mjini kila mwezi kuhudhuria mahakamani. Walihudhuria mwaka mzima, na baadaye wakaambiwa kesi haina ushahidi wakarudishiwa baiskeli zao na kuachwa huru. Wakati huo hali ya maisha ilikuwa tete.
Mungu na maajabu yake, pamoja na hayo yote darasani nilikuwa nafanya vizuri sana. Tukiwa darasa la saba mwaka 2004 kuanzia mwezi wa sita, shuleni waliweka utaratibu wa kuishi kambini shuleni ili kujiandaa na mtihani wa darasa la saba. Kuna mahitaji ambayo tulitakiwa kuchangia. Baba yangu mlezi alijitahidi lakini hakufanikiwa kuchangia vyote ambapo nilikuwa na madeni ya kutokamilisha michango ya kambini na mimi ndio nilikuwa mwanafunzi pekee niliyeshindwa kabisa kukamilisha michango.
Kulikuwa na utaratibu wa siku ya Jumapili kwenda nyumbani na kurudi jioni. Siku moja niliporudi jioni mwalimu anayesimamia kambi akatuita wote na kusema ‘hivi wanafunzi ambao hamchangii chakula tuwafanye nini? Maana huo ni unyonyaji wa nguvu za wenzenu, au muwe mnakunywa uji bila sukari? Au muwe mnakula ugali bila maharage?’ mwalimu alitumia wingi lakini mhusika ni mimi pekee na maneno yale yalikuwa yangu. Alikuwa anatimiza wajibu wake na wala hakuwa na kosa. Nililia sana siku ile na nikaondoka na kwenda darasani ambako mwalimu mwingine alikuwa akiandika ubaoni.Niliingia na kuanza kuandika. Mwalimu akauliza kwanini nipo darasani wakati wengine wanakula, nikajibu kwamba nimeshiba. Wasichana wawili waligundua kuwa nimetoka pale baada ya maneno ya mwalimu. Hivyo baada ya kuchukua chakula walichukua sahani nyingine na kunipunguzia. Wakaanza kuniita ili nikale, nilikatataa kwa aibu na maumivu lakini waliendelea kunisihi nikachukua chakula kile na kula. Mungu awabariki sana.
Niliishi hivyo hadi nikafanya mtihani wa darasa la saba! Na katika kipindi chote mguu wangu haujawahi kuvaa kiatu tofauti na makobasi (yale yanayochongwa na wamasai) ambapo kwa mara ya kwanza mguu wangu ulivaa kiatu kwenye mahafali ya darasa la saba mwezi wa kumi 2004 baada ya kununuliwa na bibi viatu aina ya njumu. Hata hivyo niliviuza mara baada ya mahafali kuisha maana kilikuwa ni kitu kigeni miguuni mwangu.
Matokeo yalipotoka nilifaulu vizuri. Swali likaja naendaje kusoma? Kwenye kata yetu ya Idodi shule ni moja tu tena ni kilometa nyingi kutoa kijijini kwetu na gharama ya mahitaji ya shule na kulipia bweni ni kubwa tusiyoimudu. Nililia sana, wenzangu wote mwezi Januari 2005 walienda kidato cha kwanza mimi nikabaki. Nilikuwa ni mtu wa kujificha ndani na kulia kwa uchungu, badhi ya watu walirusha dhihaka aina ambazo zilifanya mwili wangu kudhoofu sana. Mwezi wa nane 2005 nilienda Iringa mjini kwa mama yangu mdogo nikajaribu kutafuta kazi. Nilikuta anashirikiana na mama mmoja kuoka mikate. Moja kwa moja nilianza kushirikiana nao huku nikifanya kazi kwa bidii kwelikweli.
Mwaka 2006 ukaingia wenzangu wakiwa wanaanza kidato cha pili mimi bado nipo gizani. Siku moja asubuhi mwezi wa pili mwaka 2005 baba (mume wa yule mama anayeoka mikate na waliijua historia yangu) aliniuliza pasipo kutarajia ‘una nia ya kweli ya kusoma?’ nikajibu ‘ndio baba!’ akasema ‘sawa, tufuatilie utaratibu uanze shule’. Tulifuatilia jina langu ofisi za elimu mkoani na tukapata kibali na taratibu za uhamisho nikahamia shule moja Iringa mjini. Akanishonea nguo za shule na kunipa mahitaji yote na baadaye akanichukua nikawa naishi naye kabisa. Mke wake na watoto wake wakanipenda kama mwanafamilia na kunisaidia kwa kila kitu.
Nikamaliza kidato cha nne mwaka 2009 na baadaye kidato cha 5&6 (2010-2012) na nikafaulu na kuingia chuo Kikuu SUA shahada ya Uhandisi wa maji (2012-16) na kuanzia mwaka 2018 nimeajiriwa na Wizara ya Maji kama Mhandisi wa Maji. Mungu kanijalia mke mwema na tumejaliwa mtoto mmoja kwa sasa (2022). Wazazi wangu nawawezesha na wadogo zangu nawalipia mahitaji ya shule.
Namshukuru Mungu kwaajili ya walionisaidia kwakuwa bila wao nisingefika hapa. Wito wangu kwa vijana walioko shule wasikatishwe tama na ugumu wa maisha bali wajitume na Mungu atawasaidia. Kwa wale wenye watoto wajitahidi kutimiza jukumu la msingi ambalo ni malezi bora kwa watoto wao. Asanteni

Upvote
10