JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kumekuwa na ongezeko la vitendo vya uvunjifu wa Haki za Binadamu ikiwemo matukio ya Watu kukamatwa, kushikiliwa bila taarifa, kupotea, kutekwa na kujeruhiwa na wengine kutojulikana kabisa walipo hadi sasa. Pia kumekuwa na ongezeko la matukio ya Ukatili wa Kijinsia na watoto ambapo siku za hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la watoto kupotea, kubakwa na kulawitiwa. Matukio haya yameanza kushamiri katika kipindi cha kuelekea Chaguzi za 2024 na 2025.
Matukio yote haya yanaonekana kukosa majibu sahihi ya Uwajibikaji wa baadhi ya Mamlaka za Haki Jinai ikiwemo Polisi, Mahakama, Magereza na vyombo vingine.
JamiiForums kwa Kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wataendesha mjadala leo Septemba 5, 2024 kupitia XSpaces kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2 Usiku. Mjadala utaangazia kuchambua hali ya Mifumo ya Haki Jinai na masuala ya Haki za Binadamu nchini.
Washiriki wakuu wa Mjadala watakuwa
Tito Magoti: Mwongoza Mjadala - Wakili
Patience Ntwina: Katibu Mtendaji - Katibu Mtendaji CHRAGG
Fulgence Massawe: Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho LHRC
Raymond Kanegene: Afisa Programu Mwandamizi LHRC
Ili kushiriki mjadala huu, fuata kiunganishi hiki x.com
Tito Magoti (Wakili):
Tume ya Haki Jinai ilitoa taarifa yake Julai 2023 ambapo ilifurahiwa na Watu wengi. Taarifa hiyo ilisheheni mambo mengi ikiwemo Ukamataji, Dhamana, Matumizi ya Jeshi katika Oparesheni za Kiraia, Upelelezi Binafsi, Maadili na Rushwa, adhabu ya kifo pia ilitazamwa, Matumizi ya Teknolojia katika Uchunguzi nk
Tume ilitoa mapendekezo ikiwemo kubadili Sheria, Mfano adhabu ya Kifo.
Kuhusu adhabu ya Kifo, mbali na mambo mengine Tume ilipendekeza mtu akikaa kwa muda mrefu gerezani bila kunyongwa apewe adhabu nyingine mfano; Kifungo cha Maisha
Sasa tulitegemea mambo hayo au baadhi ya mambo hayo tokea Mwaka jana (2023) yawe yamefanyiwa kazi.
Patience Ntwina (Katibu Mtendaji - Katibu Mtendaji CHRAGG):
Mapendekezo Ya Tume ya Haki Jinai kwa CHRAGG
Kuanzishwa kwa Divisheni Maalum ya kushughulikia malalamiko ya Wananchi kwa Tume ya Haki Jinai
Kutumia kifungu cha 6 cha Sheria kinachotutaka kwenda Mahakamani pale ambapo mamlaka fulani inashindwa kutekeleza maelekezo ya Tume ya Haki Jinai
Kuhuisha mifumo ya Utekelezaji wa Taarifa za Tume ya Haki Jinai
Tumeweka utaratibu wa kuwajengea uwezo Wanasheria wetu wa Ndani ili tuweze kutimiza pendekezo la kutumia kifungu cha 6 cha Sheria cha kuwapeleka Mahakamani Mamlaka zinazoshindwa kutimiza maelekezo ya Tume ya Haki Jinai.
Wakati tunashughulika na Muundo tumetengeneza idara ya Elimu kwa Umma na Mawasiliano ambayo ni Idara mahsusi kabisa kwa ajili ya Elimu kwa umma. Pia tunaweza kutoa Elimu kwa Umma kwa kutumia radio na televisheni ambazo zinasikika nchi nzima, pia elimu inayowafikia Wananchi moja kwa moja.
Tumeona kwamba Sheria na Katiba ipo bayana kwamba taratibu za taarifa za Uchunguzi zinawasilishwa kwa Mamlaka ikiwemo kwa Mheshimiwa Rais.
Wanaokosoa nawaomba waje Tume, sisi tunafanya mambo mengi na mengine hayapo Bayana. Sasa huwa tunatoa baadhi ya taarifa kupitia vyombo vya Habari. Na nyingine tunapeleka kwenye Mamlaka zinazohusika.
Fulgence Massawe (Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho LHRC):
Mfumo wa Haki Jinai haujawahi kuwa Perfect na umekuwa ukilalamikiwa kila siku. Lakini kila nchi imekuwa ikijaribu kutengeneza.
Mimi siamini kama Sheria zetu za Haki Jinai ni tofauti za Nchi nyingine. Lakini tumekuwa na Practice na tabia mbaya hadi Rais kuanzisha Tume ya Haki Jinai.
Sheria yetu ya Makosa ya Jinai inaeleza kabisa kuanzia namna ya kumkamata mkosaji wa Jinai. Sheria haina mapungufu, ni tabia tuu ya vyombo vya Dola, ambapo sasa hivi uhalifu unaojitokeza ni kwasababu ya tabia hizi.
Ni kipindi hiki unakuta Polisi wanatembea na Magari yasiyo na namba.
Tabia mbaya za Polisi zimefanya watu wamekosa imani na Vyombo vya Usalama. Watu wanapokosa imani hawawezi kushirikiana nao.
Hakuna haja ya Kubadilisha Sheria ya kushughulikia makosa ya Jinai, vyombo vya dola vibadilishe tabia ili kuboresha ushughulikiaji wa Haki JinaiKwa bahati mbaya Serikali yetu imekuwa ngumu kutimiza na kufuata Maelekezo ya Mahakama.
Haya yanayoendelea ingekuwa ni kama ilivyotokea miaka ya 70 huko nyuma ambapo watu kama Mwinyi walikuwa wanaachia ofisi kwa kuwajibika, sasa hivi ingekuwa hivyo lazima kungekuwa na uwajibikaji
Kuna Mkataba dhidi ya Unyanyasaji ambao Tanzania hatujauridhia, huo pamoja na ule wa Mikataba inayozungumzia suala la Upoteaji wa Watu
Kuna umuhimu wa Nchi kuridhia mikataba ya Kimataifa inayolinda Haki za Watu kama hiyo
Sheria zetu nyingi zililetwa na Wakoloni ambao walileta kwa manufaa yao, lakini baada ya kuondoka Sheria hizo zinatumiwa na Wakoloni wenye Ngozi nyeusi kwa ajili ya kuwaumiza wenzao, ndio maana ukiongea neno baya unaonekana wewe ni mchochezi na sifa nyingine za aina hiyo ambazo zinaonesha haufai
Raymond Kanegene (Afisa Programu Mwandamizi - LHRC):
Maoni yangu kuhusu utekelezaji wa Haki Jinai kumekuwa na kigugumizi licha ya kuwea kuna nia njema
Tume imefanya kazi yake, sina lawama, lakini mpaka sasa hatuna ripoti kamili kuhusu ilichowasilisha Tume
Balozi Ombeni Sefue alisema kunahitajika matumizi ya Teknolojia katika kuwahoji watuhumiwa katika Vituo vya Usalama, lengo ni kuweka uwazi juu ya yake yanayoendelea vituoni.
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kwenye Jeshi la Polisi licha ya kuwa wao wenyewe Polisi wamekuwa wakisisitiza wanaendesha Jeshi kwa weledi
Nia ya Rais aliyoiweka katika Tume ya Haki Jinai inaonekana inashindwa kutekelezwa kwa vile ilivyotarajiwa kutokana na kukosekana kwa utekelezaji
Jamii ina kiu kubwa kuhusu Haki Jinai kwa kuwa inaonesha imechoka kutokana na uhalisia kuwa tofauti na inavyozungumzwa. Ikiwezekana kuwe na ile Sheria ya kuwa na Mpelelezi binafsi
Katika vituo vingi vya Polisi changamoto kubwa ambayo imekuwa ikilalamikiwa ni hao Maafisa Wapelelezi.
Suala la dhamana na upelekezi kwa pamoja yamekuwa yuakiumiza Watu wengi kwenye hizi ngazi za chini, hilo linatakiwa kuwekwa wazi.
Patience Ntwina (Katibu Mtendaji - Katibu Mtendaji - CHRAGG):
Sisi Tume wajibu wetu ni kuwa na mazungumzo ya Serikali kwa maana ya kushirikiana na Wadau wengine wa Haki, kwani haki haichagui kwa utaifa kwamba wewe ni Mtanzania
Hatutakiwi kukata tamaa, lengo ni kuwa na taratibu nzuri za kuwa na Haki za Binadamu
Sheria ya Waraka kuhusu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya Ibara ya 4 (2) inaeleza kuwa iwapo mtuhumiwa aliyekamatwa kwa amri ya Viongozi hao aliathirikika wakati wa kukamatwaa au hakukamatwa katika njia sahihi, Kiongozi mwenyewe binafsi anaweza kuwajibika kwa kushtakiwa na sio Serikali
Hiyo ni nia ya dhati ya Serikali kuonesha kuna suala la Uwajibikaji
Ni kweli kuna kazi kubwa mbele yetu ikiwemo suala la uwepo wa Taasisi nyingoi ambazo zinahusika na suala la kukamata
Fulgence Massawe (Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho - LHRC):
Mamlaka waliyopewa Wakuu wa Miko ana Wakuu wa Wilaya kuagiza kukamata Mtu ni kama hayapo, yana taratibu zake ambazo kiuhalisia ni kama hayapo
Viongozi hao mara nyingi wanakuwa hawana heshima na Wananchi kwa kuwa hawakuchanguliwa, ni tofauti na ilivyo kwa Wabunge na Madiwani na wengineo ambao wanachaguliwa na wanaweza kuwa na uchungu na Wananchi
Uwepo wa Sheria kueleza kuwa ikitokea Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya amemkata Mwananchi kisha akakiuka, ashtakiwe yeye sio sawa, inatakiwa na yule aliyempa Madaraka aui nafasi aliyopo naye awajibike
Kumuacha Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya awajibike peke yake kwa matumizi mabaya ya cheo cha Serikali sio sahihi
Clay Mwaifwani (Mdau):
Mifumo ya Haki Jinai mara nyingi anayeumia ni Mwananchi wa kawaida kabisa, kuna mifano mingi kuhusu Tume, imewahi kutoa mapendekezo lakini hayafanyiwi kazi.
Watu kama CHRAGG ambao hata taarifa yao haisomwi Bungeni tunaenda kuwapa nafasi ya kusimamia haki zetu ikiwemo kuwasimamia Polisi, hili jambo linaweka utata
Mapendekezo ya Tume hayatekelezwi, anawesa kuondoka Rais Samia, akaja Rais mwingine akaunda Tume au akaanza mchakato uleule
Mara ngapi tumeona kina Wakili Madeleka wamefungua kesi lakini DPP ameziondoa Mahakamani
William Maduhu (Wakili - LHRC):
Katika mgumo wetu ea Kioutawala kumpeleka Mahakamani kiongozi wako kama vile Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa kutoka kwa Mwananchi wa kawaida kuna ugumu
Ukitaka kumshtaki mtu mwenye cheo cha Askari kwa kosa lake binafsi, inatakiwa ile ‘samasi’ ipite kwenye ngazi za ndani ya Jeshi la Polisi, je Mwananchi wa nkawaida anafahamu yote hayo na anaweza kuyatekeleza?
Ni ngumu sana kumshtaki kiongozi wa umma ambaye anakuwa na ulinzi, ugumu wa kumpelekea mtu huyo Mahakamani unawakatisha tamaa Wananchi
Viongozi wengi weanaofanya makosa wanajificha kwenye kivuli kuwa walikuwa wanatekeleza majukumu yao
Kumekuwa na mamlaka nyingi za kukamata Nchini, ndio maana unaweza kukuta kuna Mtu anakamatwa mnaenda vituo vya Polisi haonekani, hiyo ni kwa kuwa kuna mamlaka nyingine za ukamataji
Kuna muda tunawaonea Polisi, ni kwa kuwa wakati mwingine nao hawana taarifa
Rais Samia ameunda Tume ya Haki na ameonesha nia njema lakini changamoto imekuwa katika utekelezaji, unajua Rais ni Taasisi na suala hilo linahitaji kusimamiwa
Kama ingewezekana Polisi abaki kuwa na jukumu la kukamata, suala la upelelezi liwe katika mamlaka nyingine
Francis Nyonzo (Mdau):
Tanzania tunapenda sana kufikiri kuhusu Tume, haki inabidi iendane na Sheria, tunahitaji utawala wa Sheria sio Utawala wa Tume, tukienda na utawala wa Tume zitakuwa nyingi
Tume haitakuwa na nafasi ya kumfuata Raia aliyefanyiwa makosa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, huyu Mwananchi alitakiwa kujua haki yake na uelewa kuhusu Sheria kuwa anaweza kushitaji mtu fulali au watu Fulani kwa makosa aliyofanyiwa
Tume zitaishia kutoa ripoti ndeefu na kuubwa ambazo hazitaweza kuwa na faida kwa Wananchi
Mfano, kuna Watu wanatuhumiwa kubaka lakini danadana zimekuwa nyingi, tukienda tukitumetume inaonekana kama jambo la Haki ni jambo la Hisani wakati sio hivyo kiuhalisia
Deogratias Bwire:
Ishu kubwa ya Nchi yetu ni ile kukosa utayari kutekeleza mabadiliko makubwa, tukiwa tayari tutaweka Vyombo vya kusimamia masuala ya Haki