Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hospitali ya Muhimbili inategemewa na watu wengi na kutokana na umuhimu wake imekuwa ni hospitali ya rufaa si kwa mtindo wa kawaida bali pia kwa magonjwa ambayo yangeweza kuhudumiwa katika hospitali nyingine. Ninapoangalia suala la Health Reform ya Marekani ninajiuliza je tunahitaji kufanya mabadiliko katika sekta yetu ya afya na hasa kwa wakazi kama wa Dar?
Je, hospitali ya Muhimbili na zile nyingine za wilaya zinakidhi mahitaji yetu?
Je mapungufu yaliyopo sasa yanaweza kurekebishwa au ndio tukubali kuwa "hali ndivyo ilivyo"?
Je, kiongozi kama Kikwete ana maono ya kubadilisha mfumo wetu wa afya ili uwe people friendly, affordable na zaidi ya yote uwe ni bora katika huduma au na yeye amekubali kuwa "hali ndivyo ilivyo"?
Je, tumekuwa tunaalika wawekezaji katika maeneo mengi (makubwa hasa mawili, madini na utalii) kwanini hatujafanya jitihada ya wazi na kuvuna uwekezaji katika sekta ya afya kwa sababu zilezile na hata kubinafsisha baadhi ya hospitali ili ziendeshwe kibiashara na kiushindani?
Je, katika mipango yetu ya afya kwanini Taifa la Tanzania halina Hospitali hata moja maalum ya Rufaa kwa ajili ya watoto na magonjwa ya watoto?
Kiufupi nauliza unatosheka na mfumo wetu wa afya ulivyo sasa au hutosheki? Kama kuna mabadiliko ungependa yawepo ambayo yangehakikisha kufikika kwa urahisi, gharama nafuu na huduma bora na ya wakati ni mabadiliko gani hayo?
Je na wewe ni muumini wa imani ya kwamba "hali ndivyo ilivyo" na hivyo tujifunze kuishi kwa kile kilichopo na tusijaribu kukibadilisha tusije tukaonekana tunataka kuishi kama wazungu!?