Hali ya ndoa zetu

calvinminja

Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
25
Reaction score
16
Familia moja walifurahi sana kupata mtoto. Lakini majonzi yalianza pale walipogundua siku zinaenda lakini mtoto hawezi kutamka neno lolote, mtoto alizaliwa bubu.Siku moja ghafla wakasikia anasema bibi bibi, wote wakafurahi na kujua kuwa labda kaanza kuongea, furaha yao iliisha baada ya muda mfupi Bibi wa mtoto akafariki. Baada ya hapo mtoto akaendelea kuwa bubu. Mwezi baada ya msiba mtoto akaamka anatamka mjomba mjomba, wakafurahi tena ila furaha yao ikaisha mjomba alipofariki masaa machache baadae. Sasa ikawa wasiwasi wanaogopa mtoto asifungue mdomo. Lakini asubuhi moja mtoto akasema Baba baba, basi mzee mwenye nyumba furaha ikamuishia akanyong'onyea akisubiri kifo. Usiku hakulala. Mkewe akamuonea huruma na kumwambia 'Mume wangu samahani kwa ntakalokwambia, kiukweli mtoto huyu si wako nilichepuka na baba yake amefariki masaa mawili yaliyopita' Jamaa aliamka na kumkumbatia mkewe kwa furaha na kumsifu, 'Asante mke wangu leo ndio nimejua unanipenda kwa dhati'.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…