KERO Hali ya Nishati ya Umeme Wilaya ya Bariadi kwenye baadhi ya Taasisi za Serikali ni mbaya

KERO Hali ya Nishati ya Umeme Wilaya ya Bariadi kwenye baadhi ya Taasisi za Serikali ni mbaya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali ikiwa kwenye jitihada nzito za kuhakikisha NISHATI UMEME inapatikana vijijini kote lakini huku hali ni tofauti.

Kata ya Gilya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, taasisi za Serikali kama Shule na Zahanati hazina UMEME huu mwaka wa pili, ikiwa nguzo za UMEME zimepita kuelekea vijijini kwenye nyumba za watu binafsi.

Hali hii imefanya wadau binafsi kufanya jitihada za kufuatilia na kugundua kuwa inasababishwa na mihemko ya siasa kwa viongozi hasa Diwani kuanza kujiandalia mazingira ya kupata kura na pia hata Mbunge kushindwa kusimamia jambo hili.

Naomba suala hili liwekwe wazi na lipate kumfikia Rais.

Madudu ni mengi Mkoa wa Simiyu, kuna miungu watu tumewachoka.
 
Kwa kweli hali ya huduma ya nishati kwa taasisi za serikali zilizo ndani ndani ni shida kubwa sana.
 
Ukosefu wa nishati ya umeme katika baadhi ya taasisi za Serikali kama shule za Msingi na sekondari imekuwa kero kubwa kwani umeme umepelekwa kwenye vijiji vya mbali na kuziacha taasisi hai gizani ambapo nguzo za umeme zimepita katika taasi hzo umbali wa mita kumi tu.

Hali hii inakera na inavunja moyo watumishi kwani wengi wamekaa katika taasisi hizo kwa muda mrefu bila nishati hiyo.

Tunataka kujua tatizo ni nini hasa taasisi hizo kutowekewa umeme? Au ni siasa chafu zinazoendelea kwa kuzitenga taasisi hzo!
 
Back
Top Bottom