Hali ya Uchumi na kupanda kwa bei, Waziri Kijaji asema Bei za bidhaa za ndani ni himilivu. Waziri Mwigulu aahidi kupunguza bei mafuta ya kula na gari

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
Mawaziri wawili wako ukumbi wa mikutano wa hazina, Dar es Salaam kubwa likiwa hali ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa. Yupo waziri wa uwekezaji, Dkt. Asha Kijaji na waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba.

Zifuatazo ni nukuu muhimu
Dkt. Kijaji:
Niliagiza mamlaka zinazosimamia mwenendo wa soko la bidhaa kuchukua hatua za kisheria pale ambapo chanzo cha kupanda kwa bidhaa hizo itathibitika kuwa ni michezo ya wafanyabiashara. Mamlaka haya tumepewa kisheria kupitia sheria ya ushindani.

=> Tathmini ya kina iliyofanyika inaonesha kwamba bei ya bidhaa nyingi zinazozalishwa hapa nchini bei yake ina uhimilivu yaani stable japo zipo bidhaa chache sana kama saruji na nondo ambazo bei zao zilikuwa zimepanda kwa viwango visivyohimilika wakati tunafanya tathmini hii.

=> Kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi yetu, tathmini imeonyesha bidhaa kuwa na bei zisizo na utulivu na zisizohimilika na ndio maana tuko na wazalishaji kutoka kwenye sekta mbalimbali, sekta ya mafuta ya kula, wanaotuuzia petroli, dizeli, tunao watu wa nondo, saruji ili kwa pamoja haya tuliyoyagundua tuyaseme wote kwa pamoja kwa watanzania na lipi watanzania tujiandae.

=▷Waziri Kijaji amesema visababishi walivyogundua upandaji wa bei ni janga la Uviko-19 ambapo chumi nyingi zimefungwa na upungufu wa bidhaa katika soko la dunia kutokana na kufungwa kwa viwanda baada ya watu kufungiwa kanuni ya 'demand and supply' kutumika kuamua bei.

=▷Pia Waziri Kijaji amesema vita ya Urusi na Ukraine imechangia ikiwemo Tanzania kuagiza bidhaa kutoka katika nchi husika.

=> Dkt. Kijaji: Kuna hoja kwamba ongezeko kubwa la bei za bidhaa hizi zitokapo nje ya viwanda, tulipoongea na wenye viwanda vya saruji walisema wao hawajapandisha bei kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

KUPANDA KWA BEI YA NGANO
=> Dkt. Kijaji: Tunaagiza ngano tani laki nane kwa mwaka mmoja, sisi watanzania tunazalisha tani laki moja tu kwahiyo tunaweza tukaiona athari ilivyo kubwa, hapa tunapoagiza tani laki nane, asilimia 57 inatoka Urusi na Ukraine

MAFUTA YA KULA
=> Dkt. Kijaji: Tulishaathirika na janga la Uviko, bei ya kuagiza imeongeza hivyo bei ya uuzaji lazima kuongozeka, pia vita ya Urusi na Ukraine. Kwa wachumi wanafaahamu, hii tunaita imported inflation. Unaiingiza kutoka nje kuja kwenye nchi yako kwasababu huzalishi kiwango kinachohitajika.

=> Dkt. Kijaji: Uhitaji wa mafuta ndani ya Taifa letu kwa mwaka ni tani 650,000 huku uwezo wetu wa kuzalisha ikiwa ni tani 270,000 tu.

MBOLEA
Bei ya mbolea imeruka kabisa sio kupanda. Imeruka kwasababu ya janga la Uviko na vita. Uhitaji wa mbolea ndani ya Taifa letu ni tani laki saba kwa mwaka na sisi tuna uwezo wa kuzalisha tani elfu 30, tuna tofauti ya tani 630,000 ambayo yote tunaagiza kutoka nje.

=> Mwigulu Nchemba:
UCHUMI UMEPANDA

"Ukuaji wa uchumi kwa Tanzania ulishuka kutoka 7% hadi 4.8% na sasa uchumi umepanda hadi 4.9% huku nchi nyingine uchumi wake ulishuka hadi kufikia hasi, siwezi kuzitaja wka sababu za kidiplomasia

"Dira sahihi ya kututengenezea uchumi wetu ni kuendelea na kazi, hata itokee vita huko ulimwenguni au mawimbi ya ugonjwa wa Uviko-19, dira sahihi ni kuendelea kufanya kazi.

"Yanayotokea Urusi na Ukraine, yasitufanye tukaacha shughuli za uzalishaji na uchumi au uendelevu wa miradi ya maendeleo.

"Wenzetu wa Benki ya Dunia wanasema kama tukiendelea kuwa na uvumilivu huu uchumi unaweza kupata kwa asilimia 5.5. Pamoja na majanga, tuendelee na kazi, mambo hayatakuwa rahisi lakini hii ni dira sahihi licha ya yote yanayotokea, hata kama itatoea Covid tena.

KUHUSU BIDHAA KUPANDA BEI
"Bidhaa tunazosema zimepanda, ni bidhaa zinazonunuliwa na kusafirisha. Tunachotaka kufanya ni kupunguza makali, tukitaka kuondoa tatizo lote kabisa ni kutengeneza hatari kwa kuwa tunakabiliana na tatizo lililopo nchi nyingine lakini pia tusiruhusu uhaba wa bidhaa

SUKARI KUPUNGUZWA KODI
"Rais Samia Suluhu ameelekeza tuchukue hatua za muda mfupi na kisha tukiendelea kufanya tathimini ya yanayoendelea.

"Tutapunguza kodi ya sukari kwa kiwango si chini ya asilimia 10 kwa muda, baada ya hapo tutaangalia mwezi mmoja miwili. Tutakapokuwa tunapitisha sheria mpya ya kodi tutaangalia mambo yanaendaje

MAFUTA YA GARI, MAFUTA YA KUPIKIA TUTAANGALIA
"Kwa mafuta ya magari tutaangalia gharama zinazotuhusu kwenye mafuta tuone kiwango ambacho tutapunguza. Tutaangalia ni namna gani tunaweza kupunguza. Tutaangalia sisi taasisi ndani ya Serikali kitu gani tunaweza kupunguza.

"Timu yetu ya wataalam itakaa ndani ya wiki moja hivi inaweza kuwa wameshapata jibu kujua ndamba ili tuweze kuchukua hatua. Ukisema mafuta yameshapanda bei tuondoe fedha yote inayotengeneza barabara, itaathiri barabara ambazo zinatumia fedha hizo kutengeneza barabara.

"Kwenye mafuta ya kupikia tutaangalia namna ya kupunguza na kuja na viwango vipya vya kodi na hili tutakaa pamoja na sekta binafsi kuona tunakuja kiwango gani. Ndani ya mwezi mmoja na mwezi mmoja na nusu tutaweka viwango vipya.

Tunaangalia kwa muda huu, tutakuja na viwango vipya vya kodi, tutashirikiana na wenzetu wa sekta binafsi ili tuweze kupata kitu cha kumnufaisha mwananchi wa kawaida.

"Tutapunguza sehemu ya gharama ambayo ilikuwa inaongezeka katika vifaa vya usafiri, ili tukipunguza gharama kwenye mafuta na vifaa hivyo moja kwa moja tunaamini itashusha gharama na bei ya bidhaa nyingine.

TUFANYE KAZI HATA KAMA KUNA COVID
"Angalieni wakati wa kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19 waliwafungia ndani, waliweza kuwalisha kwa wiki moja na zaidi ya watu 100 walifariki huku wengine wakiandamana kwa ajili ya chakula.

"Hakuna ambaye anajua Covid itaisha lini au mgogoro wa Ukraine na Urusi utaisha lini.

Mawaziri wawili wako ukumbi wa mikutano wa hazina, Dar es Salaam kubwa likiwa hali ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa. Yupo waziri wa uwekezaji, Dkt. Asha Kijaji na waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba...
1649676931722.png
 
Naona aibu mimi huku, hawa walipataje uwaziri kwa kweli? Badala ya kuongelea hatua za kuchukuwa unatoa ngonjera kama unafanya kampeni ya uchaguzi. Hakuna mfanya biashara atapandisha bila sababu za msingi kila mtu anataka kuuza na kufanya biashara. Huwezi kupanga bei hiyo sio kazi ya serikali ilishawashinda miaka hiyo.

Yes tatizo la kidunia ni kweli nyinyi mnachukuwa hatua gani kama dharura milipewa pesa za Covid mkaenda kujenda madarasa wakati kazi ya pesa hizo ndio sasa kupunguza kodi na zile pesa kufidia kwenye kodi ila mkafanya nini zile pesa? mkajenga madarasa wakati ni jukumu la serikali wala halina athari za Covid.

Sasa hamjui mfanye nini. Na wewe Mwigulu usiache tufungue swaumu na hizo za number zako % za kukuwa uchumi acha ujinga mjinga wewe. Sema napunguza kodi hii na ile ili kuleta unafuu, tunakata matumizi ya serikali yasiyo ya lazima na safari punguzeni kuna njia nyingi za kubana matumizi.

Miradi ya maendelea inaweza kusubiri hali hii ipite huwezi kusema tuna shida kesho unasema nanunua ndege cash halafu unajisfia tunatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo. Kasoma wapi huyu mjinga.
 
Mawaziri wawili wako ukumbi wa mikutano wa hazina, Dar es Salaam kubwa likiwa hali ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa. Yupo waziri wa uwekezaji, Dkt. Asha Kijaji na waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba.

Zifuatazo ni nukuu muhimu
Dkt. Kijaji:
Niliagiza mamlaka zinazosimamia mwenendo wa soko la bidhaa kuchukua hatua za kisheria pale ambapo chanzo cha kupanda kwa bidhaa hizo itathibitika kuwa ni michezo ya wafanyabiashara. Mamlaka haya tumepewa kisheria kupitia sheria ya ushindani.

=> Tathmini ya kina iliyofanyika inaonesha kwamba bei ya bidhaa nyingi zinazozalishwa hapa nchini bei yake ina uhimilivu yaani stable japo zipo bidhaa chache sana kama saruji na nondo ambazo bei zao zilikuwa zimepanda kwa viwango visivyohimilika wakati tunafanya tathmini hii.

=> Kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi yetu, tathmini imeonyesha bidhaa kuwa na bei zisizo na utulivu na zisizohimilika na ndio maana tuko na wazalishaji kutoka kwenye sekta mbalimbali, sekta ya mafuta ya kula, wanaotuuzia petroli, dizeli, tunao watu wa nondo, saruji ili kwa pamoja haya tuliyoyagundua tuyaseme wote kwa pamoja kwa watanzania na lipi watanzania tujiandae.

=▷Waziri Kijaji amesema visababishi walivyogundua upandaji wa bei ni janga la Uviko-19 ambapo chumi nyingi zimefungwa na upungufu wa bidhaa katika soko la dunia kutokana na kufungwa kwa viwanda baada ya watu kufungiwa kanuni ya 'demand and supply' kutumika kuamua bei.

=▷Pia Waziri Kijaji amesema vita ya Urusi na Ukraine imechangia ikiwemo Tanzania kuagiza bidhaa kutoka katika nchi husika.

=> Dkt. Kijaji: Kuna hoja kwamba ongezeko kubwa la bei za bidhaa hizi zitokapo nje ya viwanda, tulipoongea na wenye viwanda vya saruji walisema wao hawajapandisha bei kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

KUPANDA KWA BEI YA NGANO
=> Dkt. Kijaji: Tunaagiza ngano tani laki nane kwa mwaka mmoja, sisi watanzania tunazalisha tani laki moja tu kwahiyo tunaweza tukaiona athari ilivyo kubwa, hapa tunapoagiza tani laki nane, asilimia 57 inatoka Urusi na Ukraine

MAFUTA YA KULA
=> Dkt. Kijaji: Tulishaathirika na janga la Uviko, bei ya kuagiza imeongeza hivyo bei ya uuzaji lazima kuongozeka, pia vita ya Urusi na Ukraine. Kwa wachumi wanafaahamu, hii tunaita imported inflation. Unaiingiza kutoka nje kuja kwenye nchi yako kwasababu huzalishi kiwango kinachohitajika.

=> Dkt. Kijaji: Uhitaji wa mafuta ndani ya Taifa letu kwa mwaka ni tani 650,000 huku uwezo wetu wa kuzalisha ikiwa ni tani 270,000 tu.

MBOLEA
Bei ya mbolea imeruka kabisa sio kupanda. Imeruka kwasababu ya janga la Uviko na vita. Uhitaji wa mbolea ndani ya Taifa letu ni tani laki saba kwa mwaka na sisi tuna uwezo wa kuzalisha tani elfu 30, tuna tofauti ya tani 630,000 ambayo yote tunaagiza kutoka nje.

Mihogo na viazi vitamu vimepanda bei na vyenyewe vinatoka Urusi??
 
Hapo wanasubiri posho ziingie mifukoni mwao kwa hoja hizo? Sababu nyepesi kwa masuala mazito yanayohusisha maisha ya wananchi wa kawaida wa kipato cha chini.
Hapo ni Dr's wamegundua sababu za bei kuruka?
 
Hapo wanasubiri posho ziingie mifukoni mwao kwa hoja hizo?Sababu nyepesi kwa masuala mazito yanayohusisha maisha ya wananchi wa kawaida wa kipato cha chini.

Back
Top Bottom