Habari wa Jamii Forum.
Naomba mnisaidie hapa kutokana na uelewa wangu mdogo wa masuala ya uchumi, kila siku nasikia kupitia vyombo vya habari kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu ni nzuri na uchumi unakuwa kwa kasi ya ajabu.
Tatizo langu ni kwamba mimi ni mkulima nimekopwa mahindi pia hali ya kifedha serikali ni mbaya hasa maana fedha za matumizi hazitumwi na mara nyingi.
hata zikitumwa ni kidogo,swali langu la msingi nini tofauti ya kukua kwa pato la taifa/uchumi na kukosekana kwa fedha serikalini.
Naomba kama kunamtaalamu wa masuala ya uchumi anisaidie.
Asanteni sana.