Mkuu Kyomo, ule usemi wa Cheap is always expensive haukwepeki, nafikiri ni sera nzuri tu yakupiga vita yakufanya nchi yetu shimo la taka. Ukiangalia kwa karibu utagundua utumiaji wa mafuta kwa gari kuu kuu na ule wa gari jipya ni tofauti sana. Ndio maana mataifa mengine yameamua kuweka kodi kubwa kwenye magari ya zamani (used) na kodi kidogo sana kwenye magari mapya, kwa mwananchi wa kipato cha kati kiuchumi ukijiongezea kausafiri chakavu umejipeleka shimoni, weka bajeti yako vizuri agiza kitu cha uhakika. Wasalimie mafinga.