Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu kwa Sasa Hali ya umeme inarejea katika Hali yake ya kawaida,kwa Sasa shughuli za kiuchumi zinazotegemea umeme zinakwenda vyema, Mioyo ya wananchi wajasiriamali na wafanyabiashara imeanza kuwa na Tabasamu na matumaini ya kufanya kazi muda wote,Taa ya Matumaini inawaka mioyoni mwa watu Sasa, Giza linazidi kusogezwa mbali, mitaa inazidi kuwa na mwanga na kuchangamka muda wote, sauti za manung'uniko ya umeme zinapungua na Kuisha.
Sasa Ni pongezi kwa serikali ya mh Rais Wetu mpendwa Dr Samia kwa juhudi zake kubwa za kukabiliana na tatizo hili pamoja Na shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutushushia Neema Na Baraka za Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi, ambapo hata hapa napoandika mvua kubwa inaendelea kunyesha huku niliko mkoani kwangu. Hakika serikali yetu imepambana,imejitahidi kwa nguvu zake zote, kwa nyenzo zote katika wakati wote ambao tulikuwa tunapitia katika kipindi Cha ukame wa mvua kulikopelekea kupungua kwa kina Cha maji katika mabwawa yetu ya kuzalisha umeme.
Hongera kwetu watanzania kwa mioyo yetu ya Subira uvumilivu na usikivu kwa serikali yetu kwa kipindi chote Cha changamoto hii ya umeme,kwa namna ambavyo tuliungana na kuielewa serikali yetu juu ya chanzo Cha changamoto hiyo ya umeme iliyokuwa imetokana na ukame mkubwa uliokuwa umeikumba nchi yetu.
Hata hivyo Inawezekana Kuna maeneo kukawa na kukatika kwa muda mfupi kwa umeme Jambo ambalo naamini haiwezi ikawa Kama awali,hivyo Tuwe wenye Subira na uvumilivu Kama awali huku tukiendelea kuiamini serikali yetu, maana Tumeona namna inavyo pambana pamoja na juhudi zake katika katika kukabiliana na changamoto ya aina yoyote inayojitokeza mbele yetu Kama Taifa.
Watanzania Hatuna budi Kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake kwetu watanzania kwa kutupatia Baraka na Neema ya mvua katika kipindi hiki, zitakazo saidia kumaliza changamoto hii ya umeme,Hakika Mwenyezi Mungu anatupenda Sana watanzania, Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu aendelee kulilinda Taifa letu na Wala Tusikubali mtu yeyote akatugawa kwa misingi ya udini,ukabila au ukanda. Tuwe wamoja na Tumuunge mkono Rais wetu mpendwa Dr Mama Samia Suluhu Hassan na serikali yake katika kututumikia watanzania.
Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627