Hali ya Usalama Wilayani Temeke si nzuri

Hali ya Usalama Wilayani Temeke si nzuri

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
2C2BEF7E-898C-4597-BC9A-49D9A865D3BF.jpeg

===
Anaandika Vicent Kasala Twiter

HALI YA USALAMA TEMEKE NI MBAYA! DC Jokate Mwegelo,

Salam,

Nakuandikia kwa dhamana yako kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke. Awali ya yote pole kwa majukumu ya kuwatumikia wananchi.

Mimi ni mwanachi wako katika Wilaya ya Temeke unayoiongoza nikiwa mkazi wa Kata ya Buza mtaa wa Mashine ya Maji No. 5 Kabla sijahamia mtaa huo, awali nilikuwa naishi mtaa wa Makangarawe Kata ya Makangarawe, Temeke.

Mwaka jana matukio haya yalijitokeza pia kwa kiwango kikubwa. Mimi binafsi nilikuwa mmoja wa wahanga (tazama picha), kwani nilivamiwa na kukatwa panga kichwani. Hivi sasa yamerejea tena kwa kasi kubwa!

Nimeona nichukue jukumu nikuandikie hapa kukupa 'concern' nzito ya hali ya kiusalama katika mitaa yetu tunayoishi ndani ya wilaya hii.

Pamekuwa na matukio ya kuvamiwa watu nyakati za alfajiri na kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga na kisha kuporwa vitu ikiwemo pesa, simu, nk. Matukio haya yamekuwa yakishika kasi nyakati za kuelekea sikukuu kama kipindi hiki.

Mwaka jana matukio haya yalijitokeza pia kwa kiwango kikubwa. Mimi binafsi nilikuwa mmoja wa wahanga (tazama picha), kwani nilivamiwa na kukatwa panga kichwani. Hivi sasa yamerejea tena kwa kasi kubwa!

Leo, nilijihimu asubuhi kwenda hospitali kupata matibabu kwenye Kituo cha Afya Yombo Vituka (baada ya kuwa najisikia kusumbuliwa kidogo).

Wakati nafika pale, majira ya saa 12 alfajiri, nikakutana na mtu mmoja amekuja kupata matibabu baada ya kukumbana na mikasa hiyo ya kuvamiwa na kukatwa mapanga kichwani. Ningali nikitahamaki, akafikishwa mwingine amejeruhiwa mkononi kwa panga vilevile, anavuja damu nyingi sana.

Katika mazungumzo yangu na mmoja wa wahudumu hospitalini hapo, nikaelezwa ya kwamba mpaka wakati huo kwa alfajiri ya leo peke yake, walikuwa wamefikishwa watu 7 wenye visa vya namna hiyo na kati yao wawili hali zao ni mbaya sana.

Wakati naendelea kusubiri foleni ya kuhudumiwa, akaletwa mwingine, akawa mtu wa 8 kwa idadi, leo peke yake katika Kituo kimoja cha Afya! Wote wamejeruhiwa vibaya kwa mapanga na kuporwa vitu vyao! Hawa watu wamekata watu 8 kwa mapanga just in a single day!

Hali hii haikubaliki, inatishia vikali usalama wetu wananchi. Watu 8 kwa wakati mmoja ndani ya siku moja wamemwagwa damu yao na kuachwa na majeraha makubwa yatakayowagharimu muda, pesa na maumivu makali kuweza kupona.

Wanaotekeleza vitendo hivi ni vijana wa kihuni wanaokuwa kwenye pikipiki (bodaboda) wakiwa wamepakizana watatu. Wanavizia watu wanaoamka alfajiri kuwahi katika mihangaiko yao na kuwavamia barabarani.

HATUA ZICHUKULIWE
Tunahitaji hatua kali kukomesha vitendo hivi zichukuliwe haraka iwezekanavyo. Kuna vikundi vya walinzi shirikishi, viko mitaani huku, wanapita na kukusanya fedha za posho zao kila mwezi katika kila nyumba.

Hatuoni jitihada za hivi vikundi katika kuzuia uhalifu huu dhidi ya binadamu. Wengi wanakusanya fedha, wanagawana halafu hawawajibiki kutekeleza majukumu yao ya kiulinzi. Tunaomba wasimamiwe watekeleze wajibu wao ipasavyo.

Pili, matukio yote haya yanaripotiwa kwanza katika vituo vya polisi kabla muhanga hajakwenda hospitali kupata matibabu. Hii ina maana polisi wanafahamu fika uwepo wa matukio haya.

Polisi wanafahamu mwenendo wa hali ya uhalifu huu, kwamba hivi sasa umeshamiri na kushika kasi hasa kuelekea Sikukuu. Nasikitika, pamoja na ukweli huo bado hatuoni jitihada za dharura na za makusudi za kukabiliana na vitendo hivi ili kuvikomesha.

Hatuoni hata doria za polisi mitaani za maana kuwasaka wahalifu hawa. Tunaomba kuona mabadiliko haraka iwezekanavyo. Dhima ya kwanza ya dhamana ya uongozi ni maisha na usalama wa watu. Usalama wetu uko hatarini.

Asante.
Vicent Kassala,
Simu: 0719847032

Pia Soma:
- DC Jokate Mwegelo atoa siku saba kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao
 
Anamwambia nani na wakati yeye ndio mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ana mpaka RPC etc , matgatizo ya kugawa uongozi kwa kuangalia vitu vya katikati, anatakiwa awaamrishe amani irudi eboh! wanafikiri uongozi ni kupigiwa saluti tu eeh, pole yake sana
 
HATUA ZICHUKULIWE
Tunahitaji hatua kali kukomesha vitendo hivi zichukuliwe haraka iwezekanavyo. Kuna vikundi vya walinzi shirikishi, viko mitaani huku, wanapita na kukusanya fedha za posho zao kila mwezi katika kila nyumba.

Hatuoni jitihada za hivi vikundi katika kuzuia uhalifu huu dhidi ya binadamu. Wengi wanakusanya fedha, wanagawana halafu hawawajibiki kutekeleza majukumu yao ya kiulinzi. Tunaomba wasimamiwe watekeleze wajibu wao ipasavyo.

Pili, matukio yote haya yanaripotiwa kwanza katika vituo vya polisi kabla muhanga hajakwenda hospitali kupata matibabu. Hii ina maana polisi wanafahamu fika uwepo wa matukio haya.

Polisi wanafahamu mwenendo wa hali ya uhalifu huu, kwamba hivi sasa umeshamiri na kushika kasi hasa kuelekea Sikukuu. Nasikitika, pamoja na ukweli huo bado hatuoni jitihada za dharura na za makusudi za kukabiliana na vitendo hivi ili kuvikomesha.

Hatuoni hata doria za polisi mitaani za maana kuwasaka wahalifu hawa. Tunaomba kuona mabadiliko haraka iwezekanavyo. Dhima ya kwanza ya dhamana ya uongozi ni maisha na usalama wa watu. Usalama wetu uko hatarini.

Asante.
Vicent Kassala,
Simu: 0719847032
Mkuu, 'Vicent Kassala', kwanza nakupa pole kwa majanga yaliyokupata.

Pili, nakupongeza sana kwa hatua hii uliyochukua. Ni dhahiri wewe una sifa za uongozi.

Sasa cha kushangaza ni jinsi swala hili lilivyoshughulikiwa.

Hata baada ya kuyaeleza yote uliyoeleza, ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri, bado uongozi unaonekana kutotambua uzito wa hali iliyopo.

Kuna tatizo kubwa ndani ya uongozi wa nchi yetu.
 
Mnawafukuza machinga mtaani mnataka wakale wapi? tutabanana wote hapa hapa
 
Serikali ya CCM kwenye wizi wa kura wakati wa uchaguzi wanakua na askari wa kutosha kila kituo cha kupigia kura,ila nyakati za ujambazi wa mali na maisha ya wananchi, serikali ya CCM itasema undeni ulinzi shirikishi,hakuna askari!!

Cha ajabu nyakati za uchaguzi wananchi wakihamsishana kulinda ulinzi shirikishi wa kura zao vituoni wanakatazwa na kupigwa mabomu!!
 
Mabibo walkuwa wanasumbua mida flan niko chuo, walikuwa wakishikwa wanachomwa wakaacha
Waliua ata mwanachuo mwenzang kisa wakachukua laptop na simu
 
Taarifa za kiintelijensia hawakuzipata polisi ili wazime mashambulio kabla hayajatokea?

Ila wangekua wapinzani wanataka kuandamana wiki kabla wangekua wamepata zuio kwa madai kuna taarifa za kiintelijensia kuwa kutakuwepo na uvunjifu wa amani maandamano yakifanyika.
 
Hatuoni jitihada za hivi vikundi katika kuzuia uhalifu huu dhidi ya binadamu.
Hii haiwezi kuwa ndiyo urefu wa kamba ya polisi wetu? Kwann wakati wa Simba wa Yuda hapakutokea matukio ya aina hii?
 
Back
Top Bottom