Naomba kwanza nikiri mimi ni mkazi wa Kigamboni ambaye karibu Kila siku ya Mungu natumia vivuko vya feri.
Najua sio mada mpya Sana hapa jukwaani wengine wengi wameshaijadili hapa lakini kwa msisitizo naleta hii mada tena nikiwa naamini JamiiForums ni jukwaa pana, mada za humu ndani zinasomwa na wenye mamlaka ndani ya nchi yetu pendwa.
Hali ya vivuko kadri ya siku zinavyoenda inazidi kuwa mbaya na hatarisha kwa usalama wa wasafiri wa vivuko.
Tuna vivuko viwili vinafanyakazi kwa kujikongoja; MV Kazi iendelee hivi karibuni imetoka kwenye ukarabati na kutumia mabillioni ya walipa kodi, lakini cha kusikitisha utendaji wake wa kazi unaleta maswali mengi na MV Kigamboni ndio hilo tia Maji kumuomba Mungu.
Tunaomba serikali yetu walipe uzito suala la vivuko na haswa kama anavyosisitiza mbunge wetu watu binafsi wenye uwezo waruhusiwe kuleta vyombo vya kusaidia kuvuka maana Temesa wameshindwa kuendesha vivuko.
Asante