DOKEZO Hali ya vyoo Hospitali ya Sokoine, Manispaa ya Singida inatisha, viboreshwe

DOKEZO Hali ya vyoo Hospitali ya Sokoine, Manispaa ya Singida inatisha, viboreshwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Kituo cha Afya cha Sokoine ambacho wenyeji wa huku tumezoea kukiita Hospitali ya Sokoine, kilichopo katika Manispaa ya Singida ni taasisi kongwe Mkoani hapa

Kwa ukongwe wake Hospitali hiyo ilitakiwa iwe na mazingira mazuri haswaa, kuzingatia afya na usalama wa wagonjwa /wauguzaji pamoja na watumiaji wengine.

Hali ya vyoo kwenye hospitali hiyo inatisha na kusikitisha sana. Vyoo ni vichafu sana, vinatia kinyaa. Ni hatari sana kwa Afya.

Ni aibu sana kwa Hospital kama hii kuwa na vyoo kwanza vya kizamani pili na la muhimu ni vichafu mnooo.

Wahusika hebu boresheni mazingira haswa huko vyooni ambako ni kwa muhimu sana.

ZINGATIENI AFYA YA WATEJA WENU. KWAKUWA NINYI HAMTUMII VYOO HIVYO HAIMAANISHI MSIZINGATIE USAFI WA WATU WENGINE.
20241203_143216.jpg


20241203_142942.jpg
Snapchat-216271142.jpg
20241203_144156.jpg

Serikali yaanza maboresho ~ Serikali yaanza maboresho ya Vyoo vya Kituo cha Afya cha Sokoine, Manispaa ya Singida
 
Halmashauri hazina hela na zinalemewa sana ukijumlisha na upigaji basi matatizo kama haya hayawezi kuisha
 
Vyoo vya namna hiyo viko hospital nyingi Kuna siku nilienda hospital ya rufaa ya mwananyamala aisee kinyesi kimejaa kwenye sink mpaka watu wanajisaidia pembeni sikuweza nilitoka nikaenda kuomba kujisaidia nje ya hospital.
 
Back
Top Bottom