Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wabunge watatu leo nchini Kenya walibubujikwa na machozi baada ya Mtendaji Mkuu wa chama cha Madaktari Chibanzi Mwachonda kusimulia madhila yaliyowakuta baadhi ya madaktari waliopoteza uhai wao wakipambana na ugonjwa wa COVID-19.
Chama hicho cha madaktari kimelalamika kuwa ukosefu wa posho na huduma za afya kwa wahudumu wa afya kunasababisha wengi wao kukosa msaada kwa wakati, kwa mfano daktari mmoja alifariki wakati akingojea kuhamishiwa Nairobi kutoka Eldoret kwani hakukuwa na kitanda cha ICU.
Hali hiyo ilipelekea wabunge watatu kutoa machozi na kuilaumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia madaktari ambao wapo mstari wa mbele kupambana na janga hili la virusi vya corona.
Wote sisi ni wana wa Afrika ya Mashariki, tunawaombea Mwenyezi Mungu awavushe salama katika hili janga ndugu zetu wa Kenya ! 🙏 🇰🇪