Yaani kwa sasa shamba imekua changamoto. Mtu unahitaji DAP , bado UREA ongeza na CAN hapo madawa. Mafuta kwa ajili ya kumwagilia ! (Gharama za trekta na vibarua) Wengine mito tunayotumia imefikia hatua inabidi tupangiane siku za kumwagilia [emoji23][emoji23] maana maji yamekua kidogo sana au labda uamke usiku sana. Na bei ya mazao kwa kweli haiendani na gharama za uendeshaji ona Nyanya mwaka huu, Pilipili hoho , Nyanya chungu afadhali Maharage yanatubeba.
Kwa nilivyowaza mimi Bustan naipumzisha yale mashamba nayarudisha kizamani nitatia samadi ya kutosha kisha yanakaa mpaka mwezi may ndo nayafufua tena. Vinginevyo hiki kilimo tutakichukia