Hali yazidi kuwa tete kwa wakulima, mbolea kg 50 yafikia Tsh. 140,000

Ndugu zangu habarini, kuna kitu kinanisononesha Sana katika vipaumbele vya serikali ili kumletea mwananchi maendeleo, naona vipaumbele vikuu ni miundombinu ambayo mwisho wa siku huwezi kuigeuza kuwa chakula, hatuwezi kula daraja la Salenda, wala hatuwezi kula ndege zilizoagizwa na zilizonunuliwa, wananchi hawawezi kuzigeuza kuwa ugali au kitoweo nafikiri ni anasa tu.

Inanisikitisha Kama tuna pesa ya kununua ndege cash lakini hatuna pesa ya kuagiza mbolea ili kusaidia kilimo Cha nchi hii, waziri mkuu anasema wananchi wanaoingiza mbolea kutoka nchi jirani wasizuiwe swali ni je hizo nchi jirani zinatoa wapi hiyo mbolea,,tuacheni utani huu ni msimu wa kilimo unaoweza kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea Jana nilikuwa rukwa wilaya ya kwela mbolea ni 140,000 tafakari
 
Alie shiba hamfikiliii mwenye njaaa mkuu acha tupambane na hali zetu ukisema unaitwa sukuma gang.Ila tutafika tu si mda mrefu maana ukitaka kujua hasira ya mtu imkute njaaa
 
Lete manenooooo! (In JK's voice!)
 

Mda Ukifika Tutaongea Lugha Moja
 
Mkuu kama uko eneo ambalo samadi inapatikana kwa urahisi fanya hivyo.
Samadi ni rahisi sana kwa nilipo !! Kinachowashtua wakulima ni ile effect yake huwa inachelewa kidogo !! Sio kama hizi za kisasa
 
hivi ile ya pale minjingu ni mbolea gani mkuu.
Minjingu ni ya kiwandani zamani ilikuwa inachimbwa tu na kupakiwa kwenye mifuko bila maboresho sana.

Mwamba/mchanga uliopo una phoshate pekee, kwa hio ilikuwa ni kwa ajili ya kupandia tu. Na kwa kuwa haijawa refined, ufanyayi kazi wake ni taratibu sana, kwa miaka ya mwanzo unaweza sema kama unakuwa haujaweka mbolea.

Kwa sasa wameboresha kwa kuichakata katika muundo wa kuchukuliwa moja kwa moja na mizizi. Pia imeongezwa virutubisho vingine vikuu vya mmea; potassium na nitrojen ili kutengeneza NPK kamili.
 
Eti serikali ya wanyonge???
Hii sio serikali ya wanyonge wewe, ni ya wawekezaji zaidi sahizi tunaenda na mama mpaka 2035!
Mama anafungua nchi!

Mwacheni mama achape kazi jamani😅 mkimzingua atawazingua zaidi.

Yule jamaa alipokuwa anapambana mlimuita kichaa jiwe 😅dhalimu anachukia matajiri 😅 haya sasa pambaneni huyu tulie nae anapenda matajiri!
 
Hawa jamaa bila kuwafanyia uchizi tutaendelea kulalamikia kwenye forums kama hivi
 
Jamani ila mama tunamlalamimia bure tu

Bora huyu wakupandisha bei kila kitu,magufuli alitunyima uhuru wa kuongea na aliongoza nchi kidikteta sana bora huyu anatupandishia bei anatupa umeme wa mgao lakini tupiga story kijiweni tukimsema hana shida yaani nchi imekuwa na demokrasia.

Tuna uhuru wa kuongea nadhani hili ni lamsingi zaidi kwa watanzania.
 
shukran mkuu ..
 
Habari za kazi Wana JF/wadau/wananchi? Huku kwetu DAP ni laki na elfu arobaini.140,000/=hivi kwa Bei hii kilimo kitafanyika mwaka huu?

Hebu tupaze sauti, tuwasaidie wakulima hali ni Tete msimu huu.
Wavumilie tuu yule mtu wao Rais wa viwanda kwa miaka 6 ya kuimbiwa pambio alishindwa kuweka Jiwe lolote la msingi hata la kuzugia kwenye kiwanda cha mbolea.JK alijenga minjingu ila yeye bila bila kwa maneno meengi..

Hata hivyo Mama Kwa miezi 7 ameshawishi wawekezaji 2 wanajenga viwanda vikubwa vya mbolea Dodoma na Mtwara kwa hiyo wavute subira next year mbolea itapatikana kwa bei nafuu..

Samia kazini 👇







 
Hawa jamaa bila kuwafanyia uchizi tutaendelea kulalamikia kwenye forums kama hivi
Sisi ni wasahaulifu kwanza sasa hivi tushazoea mgao wa maji wala hatulalamiki tena. Wazo week ya 2 hakuna maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…