Hali yetu katika mahusiano kwa mujibu wa sensa 2022

Hali yetu katika mahusiano kwa mujibu wa sensa 2022

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Sensa 2022: Ndoa Zimeongezeka Kiduchu, Talaka, Kutengana Juu

💍Wanandoa- 51.4%

💃Hawajawahi kuoa au kuolewa- 32.9%

🛖Wanaishi Pamoja - 5.5%

😢Wajane na Wagane- 4.7%

💔Waliotalakiana- 3.7%

❤️‍🩹Waliotengana- 1.8%

Taarifa za sensa za mwaka 2022 zinaonesha ndoa zimeongezeka kutoka asilimia 51.1 ya watu wote wenye umri wa kuoa na kuolewa kwa takwimu za sensa mwaka 2012 mpaka asilimia 51.4 kwa sensa ya 2022.

Hata hivyo idadi ya watu kupeana talaka imeongezeka kutoka asilimia 2.9 mpaka asilimia 3.7 kwa sensa ya 2022. Huku pia idadi ya watu kutengana ikiongezeka kutoka asilimia 0.9 ya idadi ya watu mpaka asilimia 1.8.

Idadi ya wajane na wagane imeongezeka pia kutoka 3.1% kwa sensa ya 2012 mpaka asilimia 4.7. Wajane ni wengi zaidi ukilinganisha na wanaume waliofiwa na wake zao.
 
Back
Top Bottom