Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amesema mikopo ya kausha damu pamoja na urahisi wake wake wa kupatikana ina gharama kubwa. Akitolea mfano, amesema mtu akikopa 50,000 anakatwa 5,000 ya fomu, 5,000 nauli ya mkaguzi kuja kukagua mali zako na marejesho ya jumla ya 75,000 hivyo jumla kufanya matumizi ya 85,000 kwenye mkopo.
Akiongea na wanawake wa Kigamboni, amesema mikopo hiyo inawakausha na kuwafedhehesha. Bulembo amesema kila siku wahusika wanatakiwa kupeleka 2000.
Bulembo amewataka wanawake wakakope kwenye mikopo ya halmashauri kwani ipo na inatolewa. Halima amesema kuanzia sasa, wahusika wakitaka kutoa mikopo wafike kwa Mkurugenzi ikapitishiwe huko ikithibitika ina namna nzuri na bora kwa kina mama japo Bulembo amesema asingependa iendelee kabisa.
Kwa msaada wa Mwananchi