Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwakilishi wa wabunge wachache bungeni, Halima Mdee, amesema Dk Faustine Ndugulile, aliyekuwa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, alisimama kidete kwa wananchi wake na Taifa, kusema kweli bila kujali gharama.
"Dkt. Faustine Ndugulile alikuwa siyo mnafiki kama akiwa na jambo lake, alikuwa ni aina ya kiongozi ambaye alitumia muda wake mwingi katika kuwawakilisha Wananchi wa Kigamboni lakini kwa kazi zake za Kitaifa, alikuwa anasema kweli tupu pasipo kujali itamgharimu nini"
“Kama jambo ni nyeupe atasema nyeupe, na kama ni bluu atasema bluu, alipambana kwa ajili ya kile alichokiamini, jambo lililomletea changamoto kadhaa, lakini lilimpa heshima kubwa, inawezekana hatukumuelewa kipindi kile, lakini tumekuja kumuelewa. Taifa lilimuamini na kumchagua kuwa mwakilishi wa Tanzania katika WHO Kanda ya Afrika, na akashinda,” amesema Mdee.
Ameongeza kuwa Dk Ndugulile alikuwa mtu wa ‘moto’ aliyepaswa kuigwa na wote, akisisitiza umuhimu wa kuwa na msimamo ili kusaidia kuinua Taifa. “Watu wengi tunakuwa baridi au vuguvugu ambao ni unafiki, lakini yeye alikuwa wa moto,” amesema Mdee.